******************************
Na.Catherine Sungura,Dodoma
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kujifunza kuhusu Masuala ya Ugonjwa wa UVIKO-19 ili kuweza kuwafafanuliwa wananchi wao.
Hayo yamesemwa leo na Dkt.Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa semina ya wabunge kuhusu Corona iliyoandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
Akiongea wakati wa semina hiyo Dkt.Tulia amesema Kuwa Wabunge Kama wawakilishi wa wananchi nafunzo hayo ni Furaha Kwao kujifunza masuala ya ugonjwa huko ikiwemo uvaaji sahihi wa barakoa na umuhimu wa Chanjo.
“Sisi wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi mafunzo haya ni Fursa kwetu ya kujifunza kuhusu masuala ya UVIKO-19 ikiwemo uvaaji sahii wa barakoa na umuhimu wa kuchanja”Alisema
Dkt.Tulia aliongeza kuwa wanalo jukumu kila mmoja la kujifunza zaidi ili kuweza kusaidia jamii kuondokana na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kwenye maeneo Yao.
Hata hivyo Naibu Spika huyo alisema wataendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa Chanjo,uvaaji sahihi wa barakoa na afua nyingine za kujikinga kwani wamejengewa ujasiri wa nini waongee kwa wananchi.
Wakati huo huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima alisema kuwa hawajazifuta Tiba asili/mbadala bali wao Kama Serikali wanazibeba afua zote mbili ya Tiba asili na Chanjo ya UVIKO-19.
“Hatujazifuta Tiba asili katika kukabiliana na ugonjwa huu,tiba asili ni matibabu wakati tayari unaumwa Ila Chanjo ni kinga ya usiambukizwe au ukiambukizwa ugonjwa uwe mwepesi”Alisisitiza
Dkt.Gwajima alisema Kama Wizara wamejipanga kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuendelea kujikinga na utoaji wa Chanjo kwa kila Halmashauri kwa kushirikiana na TAMISEMI.
Naye,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo alisema kuwa ujumbe Mkubwa ni kwamba Mtu ambaye hatochanjwa yupo katika hatari kubwa zaidi pindi atakapopata ugonjwa huo.
Mhe.Nyongo amempongeza Waziri wa Afya kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendelea kupambana kwa kutoa elimu ya kujikinga kwa wananchi.