Msimamizi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) Bw.Christian Nabora (kulia)akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara namna wanavyopima magari kwa kutumia matambo maalumu na kuweza kugundua kasoro iliyopo kwenye gari lililokuwa na kasoro mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) Bw.Christian Nabora (wa kwanza kushoto)akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara namna ya kugundua gari lililokuwa na kasoro kupitia kompyuta maalumu baada ya kufanyiwa ukaguzi katika mashine maalumu mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) (kushoto) akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara kuhusu namna engine ya ndege walionayo inavyosaidia kufundisha wanafunzi wa chuo hicho kwa vitendo mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) (kushoto) akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara kuhusu moja ya mfano wa ndege ambayo hutumika kufundishia wanafunzi kwa vitendo katika Chuo hicho mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara akizungumza na watumishi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam kuona ni namna gani wanatoa mafunzo.
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Prof. Zacharia Mganilwa akizungumza mara baada Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam na kuona ni namna gani chuo hicho kinatoa mafunzo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)