Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi alipofika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, viongozi wengine wa Wizara na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Saidi pamoja na ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika ofisi za wizara jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi alipofika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akionesha kitabu chenye masuala ya historia ya Muungano ambacho amekabidhiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi alipofika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusu masuala ya elimu yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam
…………………………………………………………..
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako Septemba 3, 2021 Jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Sekta ya elimu ikiwemo kuendeleza ushirikiano katika kutoa Elimu bora Nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri Ndalichako amesema ni vizuri kuendeleza misingi ya ushirikiano katika masuala ya Elimu ikiwa ni kudumisha Muungano na kwa pamoja kuendelea kutoa wahitimu wenye ujuzi stahiki kulingana na mahitaji ya Taifa kwa ujumla.