Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Huduma Pamoja katika Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, leo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw.Macrice Mbodo akielezea huduma zinazopatikana katika Vituo vya Huduma Pamoja kwenye ofisi za Shirika hilo wakati wa kikao cha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na waandishi wa habari (hawapo pichani), leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimuelezea jambo Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo alipotembelea kaunta za watoa huduma pamoja katika ofisi za Shirika la Posta Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula akizungumza katika kikao cha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na waandishi wa habari (hawapo pichani), leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika moja ya kaunta ya watoa huduma pamoja katika ofisi za Shirika la Posta Tanzania, wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Huduma Pamoja, leo jijini Dar es Salaam. Aliyeongozana nae (nyuma) ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Macrice Mbodo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzindua Huduma pamoja(one stop center) katika ofisi za Posta Makao Makuu Jijini Dar es Salaam Septemba 6, 2021.
Akitoa taarifa ya uzinduzi huo mbele ya wanahabari Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile amesema huduma zitakazotolewa na posta ni pamoja na BRELA,NIDA,TRA,NHIF Na RITHA ambapo uzinduzi huo ni sehemu ya maboresho ya miundombinu na shirika zima kwa ujumla kutoa huduma zake kidigital.
“Shirika la Posta sasa litatoa huduma za taasisi nyingne za serikali ikiwemo huduma za RITHA,NIDA,NHIF,TRA na huduma za halmashauri mbalimbali.Tunaendelea na mikakati ya kuongeza huduma za taasisi nyingine hivi sasa huduma hizi zitatolewa Dar es Salaam na Dodoma”. Amesema Dkt.Ndugulile.
Aidha Waziri Ndugulile amesema Tanzania imeshinda nafasi mbili katika baraza la utawala wa mashirika ya posta Duniani na baraza la uendeshaji wa huduma za Posta Afrika ambapo Tanzania itakuwa sehemu ya mtoa maamuuzi.
Kwa upande wake Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw.Macrice Mbodo amesema tokea kuanza kwa mchakato wa mabadiliko,shirika limepata faida ya zaidi ya Bilion 3 badala ya hasara iliyokuwa ikizalishwa awali.
Aidha amesema kupitia maboresho hayo wateja watapata taarifa za mizigo na vifurushi vyao kwa kila hatua itakayofikia na kufikishiwa mpaka mlangoni kwake.