Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati akijiweka tayari kuanza mchezo wa mpira wa miguu mara baada ya kukamilisho zoezi la awali kuweka mwili sawa kwa ajili ya mchezo huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati akijiweka tayari kuanza mchezo wa mpira wa miguu mara baada ya kukamilisho zoezi la awali kuweka mwili sawa kwa ajili ya mchezo huo.
…………………………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma -Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema kuna uhusiano mkubwa sana kati ya michezo hasa mazoezi ya viungo na maendeleo kwasababu yanajenga uwezo kwa rasilimali watu kuwa timamu kisaikolojia na kimwili kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Dkt. Sengati amesema hayo mapema leo hasubuhi wakati akiongoza watumishi wa kada mabalimbali Mkoani Shinyanga kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuhamasisha watumishi hao kuimarisha mwili tayari kwa kupambana na magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Corona.
‘’Haya mazoezi mimi nayapatia kipaumbele kikubwa sana na nyie mnaokuja tuendele kuhamasisha wenzetu wengi zaidi tuweze kujiunga na programu hii nzuri kwasababu pamoja na maendeleo inatuweka pamoja tunafahamiana tunatengeneza yale mazoea ya kiutumishi tunapopanga mambo mengine yaweze kwenda mbele.’’Aliongeza Dkt. Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Dkt. Philemon Sengati amewahimiza wananchi wengi zaidi kushiriki mazoezi hayo kwa kuwa mazoezi hayo ni rafiki na kila mtu kwa nafasi yake anaweza kushiriki kutokana na aina ya mazoezi hayo ambayo yanahusisha kutembea na kukimbia ikiwemo mazoezi rafiki yanayotumia muziki.
Dkt. Sengati amewashakru wafanyakazi hao kwa moyo wa kufanya mazoezi na kuwataka kuhudhuria kwa wingi katika mazoezi hayo siku nyingine ikiwemo kuwai lakini pia akawataka ata wale wananchi ambao sio watumishi wa umma kujitokeza kushiriki mazoezi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amekuwa muhamasishaji mkubwa wa mazoezi hayo na anatumia fursa hiyo kuhamasisha jamii kuendelea kufanya mazoezi ikiwemo kupata lishe bora kama hatua muhimu ya kupambana na maradhi ya corona hapa Mkoani Shinyanga.