Na Lucas Raphael,Tabora
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora, linamsaka Mzee Patric Mtahungwa (60) kwa tuhuma ya Kumbaka Mtoto wa mika (13) kwa kumrubuni kwa Pipi, Soda na miwa shambani kwake anayesoma darasa la tano katika shule ya Msingi Muhulidede kata ya Shitage wilaya ya Uyui Mkoani Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Tabora Safia Jongo alisema mpaka sasa wanamsaka popote alipo lazima akamatwe na kumfikisha kwenye vyombo vya dola.
Alisema baada ya tukio hilo alikimbia kwenye Makazi yake ambapo tukio hilo lilitokea tangu Agost mwaka huu kwa kumrubuni kwamba akimaliza shule atamuoa ili awe mke wake .
Wanafunzi huyo jina (limehifadhiwa ) baada ya familia kutoa taarifa kituo cha polisi walihoji mtoto huyo aliweza kusema ukweli kuwa alibakwa zaidi ya mara tano katika maeneo ya nyumbani kwao na hata kwenye shamba la miwa yake.
Kamanda Safia Jongo alisema mpaka sasa ameliagiza jeshi lake kumsaka popote alipo akamatwe ili hatua za kisheria zichukuliwe , kwa sababu kosa kama hilo hakumtendea haki mwanafunzi huyo.
Aidha kamanda huyo alisema vipimo vilionyesha kabakwa na huduma za matibabu zilifanyika na kuonyesha alibakwa zaidi ya mara tano, jitijada za jeshi hilo linafanyika kwa kumsaka mzee Patric Mtahungwa.
Hata hivyo alisema kwamba mpaka sasa mwanafunzi huyo anaendelea na masomo katika shule ya msingi muhulidede ambako tangu darasa la kwanza akiwa anasoma hapo.
Afisa Mtabibu wa Afya wa Zahanati ya Shitage katika Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, Joseph Bundala alisema kwamba aliweza kumpima Kipimo cha Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kipimo cha ujauzito vyote havikuwa na tatizo lolote.
Nae Diwani wa kata hiyo Katela Shigela, alisama alipata taarifa na aliweza kuzungumza na mama mzazi wa mtoto huyo kwamba alibakwa na mzee Patric Mtahungwa, alifanya jitihada ya kuwa peleka kituo cha polisi ili maelezo yachukuliwe.
Shigela alisema kitendo kilichofanywa na Patric hakikumridhisha huo ni unyama wa hali ya juu kwa kumbaka mtoto wa darasa la tano katika shule ya Muhulidede.
Kwa upande wake mama mzazi hifadhi jina hilo (Regina Maguliati )alisema anasikitishwa na mzee huyo kufanyia kitendo hicho mwanae wakati ni mwanafunzi na ana umri mdogo.
Alisema baada ya kumuhoji mtoto wake , alisema alikuwa akimrubuni kwa kununulia Pipi, Soda na miwa shambani kwake na kisha kumfanyia kitendo hicho.
Regina alisema kwamba mzee Patric Mhungwa , alimbaka mtoto wake mwenye umri mdogo bila kuona hata aibu kuona kama anaweza kuwa sawa na watoto wake nyumbani.