Muonekano wa Zahanati ya Muhuwesi
Mwekezaji wa Madini Salim Alaudin Hasham akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo
Mwekezaji wa Madini Salim Alaudin Hasham kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi wa pili kulia
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi kulia akifungua kitambaa kuashiria uwekaji jiwe la Msingi la Zahanati iliyojengwa na mwekezaji wa Madini Salim Alaudin Hasham kushoto
WANANCHI wa Kijiji cha Muhuwesi Kata ya Muhuwesi wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma wamemshukuru mwekezaji wa Madini Salim Alaudin Hasham kwa kuwajengea Zahanati katika kijiji chao kwani wamekuwa na changamoto hiyo kwa miaka mingi.
Wakizungumza mara baada ya zahanati hiyo kuwekewa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio maalum za mwenge Luteni Josephine Mwambashi wamesema wamama wamekuwa wakipoteza maisha nyakati za kujifungua kutokana na changamoto ya mazingira ya zahanati ya awali hivyo kwasasa wanauhakika wa afya zao kwani watapata huduma bora.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Zahanati hiyo Mwekezaji wa eneo hilo Salim Alaudin amesema ujenzi huo umegharimu kiasi cha million 80 na ameamua kufanya hivyo baada ya kuona adha wanayoipata wananchi wa eneo hilo pindi wanapohitaji huduma hiyo.
Naye kiongozi wa mbio maalum za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Mwambashi amempongeza mwekezaji huyo na kusema yeye amekuwa mfano wa kuigwa kwa wawekezaji wengine ambao wanawekeza katika maeneo ya wananchi wawe na kipaumbele cha kuwasaidia kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.
Zahanati hiyo inatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya elfu 20 wanatoka kwenye vitongoji 20 ambao hapo awali walikuwa wanapata shida kupata huduma za afya kutokana na eneo la zahanati ya awali kuwa chakavu