******************************
Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa amewataka wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe kujenga utamaduni wa kurasimisha ardhi ili kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo imekithiri hivi sasa katika maeneo ofauti nchini na kisha kupata fursa ya kutumia ardhi hizo kupata mikopo benki.
Rai hiyo ametoa wakati akikabidhi hati 75 kwa wananchi wa mtaa wa Lyamkena mjini hapo ambapo amesema kuwa licha ya zeozi hilo kuondoa migogoro ya ardhi lakini pia linatoa fursa nyingi kwa wamiliki, ikiwa ni pamoja na kuwa na mipango endelevu na kukopesheka na taasisi za kifedha.
“Tunatakiwa kurasimisha ardhi zetu ili zitusaidie kukabiliana na migogoro ya ardhi baina yetu ambayo imekuwa mingi kwa sasa”alisema Gwakisa.
Nae diwani wa kata ya Lyamkena Salum Mulumbe ameweka bayana manufaa wanayokwenda kuyapata kwa hatua waliyopiga ya kukata hati ya maeneo yao.
Kaimu kamishina wa ardhi Mkoa wa Njombe Frolence Kanot amesema tangu zoezi la utoaji hati lianze kufanyika 2018 imekuwa na mafanikio makubwa na kwamba watu wahamasike ili hati ziwasaidie katika mambo mbalimbali huku wananchi nao wakionyesha hisia zao.