TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA NA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA
Kufuatia kukamilika kwa uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bibi Sophia Elias Kaduma na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Bw. Florence M. Turuka uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi za taasisi hizo zilizo chini ya Ofisi yake.
Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu 29 (1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:
- 1. Bw. Mbaraka Mohammed Abdulwakil – Katibu Mkuu Mstaafu;
- 2. Jaji Crecencia William Makuru – Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania;
- 3. Bibi Riziki Joseph Kuhanwa – Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo Mstaafu wa Ofisi
ya Rais; na
- 4. Kamishna Said Abeid Kamugisha – Mkuu wa Kitengo cha Sheria Mstaafu wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Aidha, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Wakala za Serikali, Sura 245, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:
- 1. Jaji Awadh Mohamed Bawaziri – Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
- 2. Prof. Masoud Hadi Muruke – Mhandisi Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Uteuzi wa wajumbe hao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 2, Septemba, 2021.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inatoa pongeza kwa wajumbe walioteuliwa na inawatakia kazi njema katika utekelezaji wa majukumu yao.