Kaimu Meneja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala Bw. Stephen Maganga, Pia ni Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Ilala akizungumza na wakazi wa Kata ya Chanika leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ilala Bw. Deusdedit Hokororo akizungumza na wakazi wa Kata ya Chanika leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Wilaya ya Chanika Bi. Mwanaisha Mbita akizungumza na wakazi wa Kata ya Chanika leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Lukoni Kata Ya Chanika jiji la Dar es Salaam Bw. Abdallah Saidi Pazi akizungumza na wakazi wa Kata ya Chanika leo ambapo TANESCO Mkoa wa Ilala walikuwa na kikao na wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Kutoka kushoto Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Wilaya ya Chanika Bi. Mwanaisha Mbita, Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ilala Bw. Deusdedit Hokororo pamoja na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Lukoni Kata Ya Chanika jiji la Dar es Salaam Bw. Abdallah Saidi Pazi wakiwa katika picha ya pamoja.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho kilichoandaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
***************************
.
TANESCO MKOA WA ILALA YAWAJENGEA UWEZO WANANCHI KUEPUKANA NA CHANGAMOTO.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala imewataka wateja wake kufata kanuni na taratibu ikiwemo kuepuka njia ambazo sio rasmi katika kupata huduma ya umeme jambo ambalo litawasaidia kuondokana matatizo siyokuwa ya lazima.
Maagizo hayo yamekuja baada ya TANESCO Mkoa wa Ilala kufanya kikao na wananchi wa Kata ya Chanika kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Akizungumza na wakazi wa Kata ya Chanika leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala Bw. Stephen Maganga, amesema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa tabia ya kuiba umeme jambo ambalo sio rafiki kwa serikali.
Bw. Maganga amesema kuwa wizi wa umeme ni kuchezea miundombinu ya serikali, hivyo ni kosa kisheria na mtu yoyote akikamatwa atafikishwa katika vyombo vya sheria pamoja na kupigwa faini.
“Ukiomba huduma ya umeme kwa mujibu wa taratibu mpaka siku 30 kwa wale ambao hawatumii nguzo, na siku 60 wanaotumia nguzo, tunatakiwa kuwa na subira wakati mnasubiri na sio kufuta njia ambazo sio za kiofisi ”amesema Bw. Maganga.
Bw. Maganga ambaye pia ni Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Ilala, amewaomba wananchi wote kutoa taarifa pale watakapobaini kuna mtu anatumia njia mabazo sio rasmi kupata huduma ya umeme.
Ameeleza kuwa endapo mtu atatoa taarifa za mteja wao anatumia njia ambazo sio rasmi kupata huduma ya umeme atapewa kiasi cha fedha, huku akisisitiza hatatoa siri ya mtu aliyemwambia taarifa hiyo.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ilala Bw. Deusdedit Hokororo, amewataka wananchi kuwa makini na miundombinu ya umeme ili kuepuka kupata madhara.
Amebainisha kuwa wapo baadhi ya watu wanatabia ya kukaa karibu na miundominu ya umeme jambo ambalo sio rafiki kutokana wanaweza kupata madhara na wao hawahusika katika kumlipa mtu yoyote fidia.
“Tukae mbali na wire za umeme, transformer kwani sisi TANESCO hatutamlipa mtu yoyote kama akipata madhara kwani ni hatari kwenu nyinyi” amesema Bw. Hokororo.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Wilaya ya Chanika Bi. Mwanaisha Mbita, amesema kuwa taratibu rasmi za kupata huduma ya umeme wateja wanatakiwa kufika ofisi za TANESCO kwa ajili ya kupata fomu na maelezo.
Ameeleza kuwa kuna idadi kubwa ya watu wakipewa taarifa ambazo sio za kiofisi na kusababisha kutapeliwa na kuleta usumbufu.
“Nenda katika ofisi yoyote ambayo ipo karibu na wewe, sisi wa Chanika tunayo ofisi zetu pale Magenge, kama mkikwama njoo mnione, hamtakiwi kumpa taarifa zako fundi njoo ufanye maombi mwenyewe”
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Wilaya ya Gongolamboto Bi. Mariam hilal, alielezea kuwa TANESCO kwa sasa inaenda na technologia na imeanzisha TANESCO APP ambayo wateja wenye simu janja wanaweza wakapakua na kujisajili kwenye mtandao huo.
Amesema kuwa TANESCO App inasaidia kupata huduma mbalimbali bila kufika ofisini, njia hii ya kuwasilisha taarifa za wateja inarahisisha wateja kuweza kupata huduma bila ya kufika ofisini.
Hata hivyo wananchi wa Kata ya Chanika wameonekana wakifurai baada ya kupata elimu kutoka TANESCO Mkoa wa Ilala kutokana itawasaidia kuepukana na changamoto mbalimbali ikiwemo matapeli.