****************************
Septemba 1
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MAMLAKA ya Udhibiti Ununuzi wa Umma PPRA imetoa mafunzo kwa wakuu wa vitengo vya manunuzi na ugavi 900 wa Halmashauri hapa nchini ili kupata uelewa zaidi juu ya masuala hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo ,wakati wa mafunzo juu ya taratibu sheria na kanuni za manunuzi ya umma ,Frank Yesaya ofisa manunuzi na ugavi ,alisema mafunzo hayo yalitolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Pia aliwataka maofisa hao kufuata Sheria za manunuzi ili kuepukana na hoja ambazo zinaweza kujitokeza wakati ukaguzi wa mikataba ya miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika halmashaurli hizo.
Awali akifungua mafunzo hayo katibu tawala wa mkoa wa Pwani , Mwanasha Tumbo aliwataka maofisa hao kusimamia manunuzi na mikataba mbalimbali ya miradi ya maendeleo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi.
Ismail Kiwela mwenyekiti wa halmashauri Chalinze,alishukuru kupata uelewa juu ya masuala ya manunuzi na namna halmashauri inavyotoa tenda na kutafuta mawakala ili kutekeleza masuala ya maendeleo.
Alisema, ni jukumu lao kuwa mabalozi wa kwenda kusimamia manunuzi na mikataba inayotolewa.