Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akikagua mfumo wa kuandikisha rejesta ya wanachama kupitia mfumo wa Tehama wakati wa zoezi la uhakiki na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Alliance for Democratic Change(ADC) jana jijiji Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa ADC, Bw. Hassan Mvungi.
Kamishna Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Bw. Donn Wazir Mwalami akimuelekeza jambo Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (CIA), Bw. Peter Lyimo wakati wa zoezi la uhakiki na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho jana jijiji Dar es Salaam.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Peter Lyimo akikagua hati za malipo za Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) wakati wa zoezi la uhakiki na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jana jijiji Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa ADC Bw. Doyo Hassan Doyo.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Alliance for Democractic Change (ADC) Taifa na baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi cha zoezi ya uhakiki wa vyama toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jana jijini Dar es Salaam. (Picha na: ORPP)