Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza akitoa maelekezo kuhusu nyaraka zinazotakiwa kukutwa katika Ofisi Chama cha Siasa kilichosajiliwa kwa Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Bw. Tozy Ephraim Matwanga wakati wa zoezi la Uhakiki wa wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam. Katikati Naibu Katibu Mkuu wa NLD Tanzania Bara, Bibi. Amina Mcheka. (Picha na: ORPP)
Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD) Bw. Tozy Ephraim Matwanga akifafanua jambo mbele ya kikosi kazi cha zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania (ORPP), walipotembelea katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto aliyekaa ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Sias, Bw. Sisty Nyahoza.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bibi. Edina Assey na Mhasibu Mwandamizi wa ORPP, Bw. Edmund Mugasha wakikagua nyaraka ya Ukaguzi wa Hesabu za Chama cha National League for Democracy (NLD) wakati wa zoezi la Uhakiki wa wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wajumbe wa Kikosi kazi hicho.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akikagua baadhi ya nyaraka za Usajili wa Chama cha National League for Democracy (NLD) wakati wa zoezi la Uhakiki wa wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD Tanzania Bara, Bibi. Amina Mcheka na katikati ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Tozy Ephraim Matwanga.
Wajumbe wa Kikosi Kazi cha zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha National League for Democracy (NLD) zilizopo Mtaa wa Weruweru, Sinza D jijini Dar es Salaam leo tarehe 31 Agosti 2021.