******************************
Klabu ya Simba Sc imetangaza siku ya uzinduzi wa jezi zao mpya za msimu ujao zinazotolewa na mzabuni wao mpya wa kampuni ya Vunja anayefahamika zaidi kwajina la Fred Vunja Bei.
Akizunguumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema jezi zitakazozinduliwa ni imara na zitaweza kupendwa na mashabiki kwani zinavutia na imara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Vunja Bei, Fred Vunja Bei amesema uzinduzi wa jezi utafanyika jumamosi Septemba 4, 2021 saa 1:00 usiku kwenye hoteli ya Hyatt Regency. Litakuwa tukio ambalo litahusisha wadau mbalimbali, pia watakuwa live kupitia Azam TV.
“Jambo moja naweza kusema ni jezi nzuri sana. Tutakuwa na jezi za aina tofauti sana kulinganisha na timu zingine za ndani. Baada ya uzinduzi jezi zitakuwepo kwenye maduka ya Vunja Bei na tutauza masaa 24.”Amesema Fred.
Nae Msanii wa Bongo fleva Whozu ametangaza wimbo mpya ambao tutautumia kwenye Simba Week, unaitwa SIMBA NI NOMA, na ameimba kwa kushirikiana na msanii Donat Mwanza.
Kwa upande wa Mwijaku amesema Simba ndio timu ya kwanza Tanzania kuweka mchakato wa jezi wazi na kuwaamini vijana. Tunaposema Simba ni kubwa tunamaanisha kwa vitendo.