Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua Kliniki inayotembea (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Pamoja nae ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui (wa pili kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman (Kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (Kushoto).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi (Kushoto) wakati akijiandaa kuzindua jengo la madarasa ya skuli hiyo yaliyojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Wengine ni pamoja na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahia pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua jengo la madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati Rais alipokuwa akigagua jengo la madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akijadili jambo na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua Kliniki inayotembea (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (Kulia) akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zawadi kwa niaba ya Umoja wa wanawake wa benki hiyo ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kutambua jitihada za Rais Samia katika kuliongoza taifa.
Monekano wa jengo la madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC.
Wanafunzi na wakazi wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wakiwa wameketi pembeni ya Kliniki inayotembea (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar
Baadhi ya wagenini waalikwa pamoja viongozi wa benki ya NBC wakifuatilia uzinduzi huo.
Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi wakitoa burudani mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
NBC Mambo poa! Ndivyo wanavyoonekana wakisema baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi walipohudhuria hafla ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Skuli hiyo lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC.