Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi Ya Furahika Education College Organization Bw.David Msuya akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chuo cha Furahika Education College leo Jijini Dar es Salaam
Wanafunzi wa Chuo cha Furahika Education College wakiendelea na masomo katika chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
******************************
TAASISI Ya Furahika Education College Organization ambayo inayotambulika na VETA imesogeza mbele nafasi za kujiunga na chuo cha Furahika Education College mpaka tarehe 15 Septemba 2021 ili kuweza kupokea wanafunzi wa kutosha katika awamu hii.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chuo cha Furahika Education college Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw.David Msuya amesema kuna halmashauri ambazo ziliombwa kupeleka watoto katika taasisi hiyo lakini mpaka sasa hawajapeleka ambazo ni halmashauri ya Manispaa ya Arusha, Masasi,Mtwara, Moshi hivyo wameombwa tena kufanya hivyo kwani nafasi bado zipo.
Amesema Chuo hicho mwanafunzi halipi ada hivyo mwananfunzi anachotakiwa kulipia ni mtihani ambao atatakiwa kulipa shilingi 80,000/= mpaka 30,000/= kwasababu ile mitihani wanaifanya ili mtoto aweze kupata cheti chake mwenyewe.
“Chuo hiki hakichukui ada, kai yeu ni kuendeleza watoto wa kike na vijana kuwapa ujuzi mbalimbali kwaajili ya mafanikio yao na wale ambao watawahi kufika chuoni watapewa hosteli bure kwaajili ya kulala wakiendelea na masomo yao”. Amesema Bw.Msuya.
Aidha maewataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika chuo hicho ambao wamemaliza elimu ya msingi na sekondari mwaka jana na mwaka huu kuja kujifunza kwani ni njia pekee ya kuunga mkono juhudi za serikali kuwajari watoto wakike.
“Kupitia kusoma kwa mtoto wakike kutamsaidia mtoto kujiepusha na tamaa na ushawishi mbalimbali majumbani na kumfanya mtoto asishike ujauzito kwani atakuwa bize na masomo shuleni”. Amesema Bw.Msuya.