***************************
Chama cha mchezo wa Karate Tanzania (TASHOKA) Weekend hii kinatarajia kuendelea na Mashindano ya Mchezo wa Karate ya (Ndondo Karate Championship) katika maeneo ya ilala Boma Jijini Dar Es salaam (Ukumbi wa Klabu ya Serengeti)
Mashindano hayo yenye Lengo la kukuza vijana wa mchezo huo kuanzia ngazi ya nchini ya Mchezo huo,na hatimaye hapo baadaye vijana hao kuiwakilisha Tanzania Katika Mashindano Mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa karate nchini Tanzania, Sensei Yahaya Mgeni amesema,aina ya mashindano hayo ya (Ndondo Karate Championship) pia yanafanyika katika mikoa mbalimbali Nchini Tanzania.
Hii ni Mara ya kwanza kufanyika kwa aina hii ya mashindano nchini Tanzania (Ndondo Karate Championship),na pia chama cha mchezo wa karate kina mpango wa kuwatumia mabingwa wa mashindano hayo katika Mashindano ya Nyerere Day mwezi wa 10 mwaka huu,na Baada ya mashindano hayo, hapo baadaye Kutakuwa na mashindano ya Makarateka wazoefu wa mchezo huo kwa lengo la kuzidi kuufanya mchezo huo kukua nchini Tanzania .