Mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo akizungumza kwenye kikao kazi na wanawake vinara wa lishe bora namna ya kutafuta njia ya kutatua tatizo la udumavu mkoani Iringa
Baadhi ya wanawake vinara wa lishe bora wakiwa makini kumsikiliza meneja wa shirika lisilo la kiserikali la
Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza wakati semina ya kukabiliana na udumavu mkoani Iringa.
Mkoa wa Iringa umeziagiza
halmashauri zote kuhakikisha zinatenga na kutoa fedha kwa ajili ya kupambana na
tatizo la udumavu ambalo limekuwa linaleta doa licha ya mkoa huo kuwa mmoja ya
mikoa ambayo inaongoza kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula.
Akizungumza kwenye mkutano na
wanawake vinara wa halmashauri tatu za mkoa huo,mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa kumekuwa
na changamoto ya utolewa wa fedha kutoka kwa wakuu wa Idara mbalimbali za
Halmashauri na kukwamisha mpango wa serikali ya mkoa kukabiliana natatizo la
udumavu.
Alisema kuwa serikali haitasita
kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa mkurugenzi yeyote yule atakayekaidi
agizo la kutoa fedha hizo kwa ajili ya kupambana na udumavu katika ngazi zote
za halmashauri kama ilivyopangwa.
Moyo alisema kuwa haiwekani
Halmashauri zote zimefanikiwa kutenga asilimia kumi kwa ajili ya makundi maalum
ambayo ni vijana,wanawake na walemavu na kusindwa kutenga bajeti kwa ajili ya
mpango wa uelimishaji jamii kuhusu lishe bora jambo ambalo linasababisha mkoa
wa Iringa kuwa kinara kwa tatizo la udumavu.
“Mimi kama mkuu wa wilaya na
kwa niaba ya mkuu wa mkoa nwa Iringa Queen Sendiga hatuweze kuendelea kuona
tatizo la udumavu likiendelea huku wakurugenzi wakeindelea kuzembea kutenga na
kutoa bajeti kwa ajili ya elimu ya lishe bora” alisema Moyo
Aidha Moyo amewaasa wanawake vinara ambao walishiriki mafunzo
lishe bora kuhakikisha wanaitumia vilivyo elimu waliyoipata kuhusu maswala ya
lishe na kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii juu ya malezi stahiki ya watoto
ikiwemo swala uzingatiwaji wa lishe bora.
Alisema kuwa anaamini kuwa
wanawake ni jeshi kubwa hivyo wakiungana katika mapambano dhidi ya udumavu
itasaidia kwa kiasi kikubwa kupuza au kumaliza kabisa tatizo la udumuvu na
kuundosha mkoa wa Iringa katika aibu ya kuwa kinara wa tatizo hilo.
Moyo aliwataka watendaji wa
Halmashauri zote za mkoa huo kuhakiksha wanapoanda mpango kazi wowote
wahakikishe wanaweka agenda ya lishe inayolenga kuushusha mkoa wa Iringa katika
nafasi ya udumavu ambao mkoa upo kwa hivi sasa ukiwa na kiwango cha asilimia 37.
Akizungumza kwa niaba ya
wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa wa Iringa,mkurungezi wa Halmashuri ya
manispaa ya Iringa Limbe Limbe alisema kuwa ameyapokea maagizo hayo na
atayafikisha kwa wakurugenzi wote ili kuhakikisha mkoa wa Iringa unaondokana na
tatizo la udumavu ambao limekuwa likiutia doa mkoa.
Limbe alipoungeza mradi wa USAID
lishe endelevu unaotekelezwa kupitia
shirika la Diloitte kwa kuwezesha mafunzokwa jamii wakiwemo wanawake vinara wa
Halmashauri tatu za mkoa wa Iringa kukabiliana tatizo la udumavu akitaja kuwa
mpango huo ni chachu ya kufikia malengo ya kutokeza tatizo hilo.
Kwa upande wake meneja wa shirika lisilo la kiserikali la
Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza alisema
kuwa lengo la walisha hiyo ni kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha wanatafuta
namna ya kufikisha elimu ya lishe kwa jamii kwa ujumla.
Alisema
kuwa wanawake vinara wa lishe wanauwezo mkubwa wa kufikisha elimu ya lishe kwa
jamii kwa kuwa wanawake ndio wamekuwa nguzo ya familia katika mpangilio wa
chakula kwenye familia nyingi za kitanzania na afrika lkwa ujumla.
Masenza
alisema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na maradi wa lishe endelevu
unaofadhiliwa na USAID kupitia shirika lisilo la kiserikali la Diloitte ambalo
lengo lao kubwa ni kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanakuwa na elimu ya
lishe bora ili kuondokana naudumavu uliopo.