********************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ni moja ya vituo 550 vya chanjo ya UVIKO — 19. Kabla ya chanjo Taasisi kupitia Prof. Mohamed Janabi na madaktari wengine huwa inatoa elimu ya chanjo na ugonjwa wa UVIKO – 19.
Kama moja ya kituo cha kutoa chanjo ya UVIKO – 19 Taasisi imekua ikitoa elimu na huduma ya chanjo kwa wananchi wote wanaotembelea JKCI kwa ajili ya kupata huduma hiyo lakini pia imefanya hivyo kwa wafanyakazi wa Tanzania International Container Terminal Services – TICTS, Shule binafsi ya International School of Tanganyika – IST tawi la Upanga na leo itafanya hivyo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.
Katika Taasisi chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum kina jumla ya vitanda tisa (9) tu, na mara zote wagonjwa wanaolazwa katika chumba hicho ni wale waliotoka katika upasuaji wa moyo tu.
Taasisi hailazi mgonjwa mwingine yeyote ICU ambaye hajatoka kwenye upasuaji. Kwa kipindi cha mwezi sasa ICU haijawahi kuwa na wagonjwa zaidi ya watano kwa wakati mmoja.
Taasisi bado inahimiza wananchi kujitokeza kwenye semina za chanjo ya UVIKO — 19 maana semina hizo zinatoa fursa ya kuuliza maswali na baada ya hapo kwa ridhaa yako utafanya maamuzi ya kuchanja.
Tunashauri wanahabari kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya UVIKO – 19 na kuendelea kuhamasisha watu kuja kuchanjwa