Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai,akichagia mada wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatili hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Leila Ngozi,akichagia mada wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKOA wa Dodoma umeidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 314 katika mwaka wa fedha 2020-2021 ambapo kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021 shughuli za Serikali zimeendelea katika kila sekta kwa mafanikio makubwa.
Sekta hizo ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Serikali ,uwezeshaji wa wananchi kiuchumi,,sekta za kilimo na vyama vya ushirika,mifugo na uvuvi,elimu,afya,miundombinu,maji,ardhi na makazi na usambazaji wa umeme.
Akiwasilisha leo,Agosti 25,2021 Jijini Dodoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi June 2021Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amesema katika mwaka wa fedha 2020-2021,Mkoa uliidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 314.
Amesema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 109 zilikuwa ni fedha za maendeleo zikihusisha fedha za ndani zaidi ya shilingi bilioni 68 na fedha za nje zaidi ya shilingi bilioni 41.
Mtaka amesema katika kipindi cha Januari hadi June Mkoa ulipokea zaidi ya shilingi bilioni 109 kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya bajeti na fedha miradi ya maendeleo zaidi ya shilingi bilioni 24.
Amesema fedha za mishahara ni zaidi ya shilingi bilioni 79 na za matumizi mengine ni zaidi ya shilingi bilioni 5 ambapo amedai katika fedha za maendeleo za ndani ni zaidi ya shilingi bilioni 18 na fedha za nje ni zaidi ya shilingi bilioni 6.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema makadirio ya makusanyo ya ndani kwa mwaka 2020-2021 yalikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 61 ambapo hadi June 2021 makusanyo yalikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 49 sawa na asilimia 81.22 ya lengo.
Amesema kwa kipindi cha Januari hadi June 2021 kiasi kilichokusanywa ni zaidi ya shilingi bilioni 19.
Mtaka amesema Mkoa umeendelea kutenga fedha kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo amedai Halmashauri 7 hupaswa kutenga asilimia 40 na Halmashauri ya Jiji la Dodoma hupaswa kutenga asilimia 60 ya mapato yake ya ndani.
Amesema katika mwaka wa fedha 2020-2021, zaidi ya shilingi bilioni 27 zilitengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri 7 za Mkoa wa Dodoma.
“Kutokana na fedha zilizotengwa Mkoa umeweza kutekeleza miradi mingi katika sekta za afya na elimu,”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa umeendelea kuwezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mafunzo pamoja na mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Amesema katika mwaka 2021,Mkoa ulipanga kusajili vikundi 584 vya wajasiriamali wadogo na kuvipatia mafunzo ambapo amedai vilivyosajiliwa ni 563 ikiwa ni sawa na asilimia 96vikijumuisha vikundi 298 vya wanawake,149 vya vijana na 51 vya watu wenye ulemavu.
Amesema Mkoa uliweka lengo la kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 ambapo hadi kufikia June mwaka huu jumla ya shilingi bilioni 2 zilitolewa sawa na asilimia 80 ya lengo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema vikundi 303 vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu ndivyo vilivyopata mikopo wa asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani katika kipindi cha Januari hadi June 2021.
Kwenye Kilimo,Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa ulikisia kulima jumla ya hekta 1,187,460 za mazao ambazo zilikisiwa kuzalisha tani 1,716,761 ambapo hekta 939,736 zimelimwa na kuzalisha tani 1,277,7 sawa na asilimia 79 ya enep lilopagwa na asilimia 74 ya malengo ya mavuno.
Amesema Mkoa umeweka mikakati ya kuongeza tija na uzalishaji wa mazao kwa uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji ambapo hekta 37 zimeendelezwa katika Halmashauri za Dodoma Jiji na Mpwapwa.
Pia,uanzishaji wa kilimo cha kitalu nyumba ambapo mashamba matatu yameanzishwa katika Halmashauri za Chamwino na Kondoa Mji.