……………………………………………………………
NJOMBE
Serikali mkoani Njombe imeipongeza kampuni iliyojipambanua katika kuhudumia wakulima ya One Acre Fund kwa kitendo cha kufungua maduka ya pembejeo mijini na vijijini ili kurahisisha na kusogeza mbolea huduma hiyo jirani kwa mkulima.
Akitoa taarifa kwa niamba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Lauteri Kanoni ambaye ni mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe katika hafra ya uzinduzi wa maduka 17 ya pembejeo mkoani Njombe na mengine 15 katika mikoa ya Mbeya na Songwe amesema kitendo kilichofanywa na kampuni hiyo cha kuleta mbolea za kupandia na kukuzia,kuwajengea uwezo wakulima kwa kuwapa elimu pamoja na kupunguza gharama za mkopo wa pembejeo kimeonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa watanzania hivyo kuna kila sababu ya kuiunga mkono kwa jitihada hizo.
Kanoni Amesema One Acre Fundi imeongeza fursa ya ajira katika jamii na kuongeza kiwango cha mapato mkoani Njombe kwasababu ujio wake umesaidia kuhamasisha wakulima wengi kuingia katika kilimo na kufanya kilimo chenye tija na mahitaji makubwa sokoni.
” Mh mgeni rasmi kampuni hii imekuwa na faida kubwa kwa mkoa wa Njombe kwasababu imetoa ajira nyingi na kusogeza pembejeo za kilimo kwa wakulima hivyo naipongeza sana kwa hatua hii”Alisema Lauteri Kanoni mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe.
Kuhusu huduma nyingine Msetti amesema ili kuwafanya wakulima wanapata mazao bora na yenye tija kampuni imekuwa ikitoa mafunzo kwa wakulima kupitia maafisa ugani zaidi ya 300 wa kampuni,kuwapa vitendea kazi,mikopo yenye riba rafiki ambayo imeshuka kutokaasilimia 18 hadi 10 huku lengo likiwa ni kumuinua mkulima.
” Kampuni ya One Acre Fund imejipanga vyema katika kufanya mapinduzi katika kilimo kwa kutoa huduma zote muhimu kwa wakulima wa mkoa wa Njombe na maeneo mengine inakohudumia kwa lengo la kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao na kuifanya nchi kuwa na hazina kubwa”,Alisema Alice Msetti
Lindgren amesema katika miaka 8 iliyopita kampuni imewekeza zaidi ya bil 56 kwa watanzania kwa njia ya kutoa mikopo kwa wakulima huku pia wakifanikiwa kusambaza pembejeo zaidi ya tani elfu 32 za mbolea na tani elfu 3 za mbolea na kufanya zaidi ya pembejeo elfu ambazo zimetolewa kwa wakulima.
” One Acre fund imedhamiria kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kusogeza huduma karibu kwa wakulima, hatua ambayo imekwenda sambasamba na utoaji wa ajira kwa watanzania kwa zaidi ya asilimia 90″Alisema mkurugenzi mkuu wa kampuni Jenipher Lindgren.
Akuzungumzia kuhusu changamoto ya soko la mahindi Malema amesema tayari serikali imesikia kilio cha wakulima na kisha kuchukua hatua za haraka ambapo imeshatangaza vituo vya kununua kwa bei nzuri ya shilingi 500 kwa kilo jambo ambalo linaleta tija kwa mkulima.
Bi Omary amesema wakulima wanapaswa kuondoa shaka juu ya utendaji wa kampuni hiyo kwasababu serikali imechunguza kwa muda mrefu na kujiridhisha na kisha kutoa pongezi kwa kitendo cha kupunguza gharaza za tozo za mikopo ya pembejeo za kilimo kutoka asilimia 19 hadi asilimia 10 huku jambo lingine ambalo limepongezwa ni kusogeza huduma vijijini kwa wakulima ya ufunguzi wa maduka pamoja elimu ya matumizi sahihi mbolea na udongo.
“Wizara ya kilimo ipo tayari kushirikiana na wadau wote hususani One Acre Fund kwasababu wameonyesha dhamira ya dhati ya kuendeleza sekta ya kilimo”,Alisema Judica Omary katibu tawala mkoa wa Njombe
Mikoa mingine ambayo imesogezewa mradi wa maduka ya pembejeo vijijini ni Mbeya na Songwe