,Njombe.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoani Njombe NJOREFA dkt Thobias Lingalangala,amechangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya kutumika kwenye usajili wa timu ya Njombe mji iliyopo mjini Njombe.
Akizungumza jana mara baada ya kutoa mchango huo ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya ,Lingalangala aliwaomba wadau wa mpira wa miguu mkoani humo kujitokeza ili kurudisha matumaini katika timu hiyo.
‘’Tuna timu yetu Njombe mji ambayo inafanya usajili sasa,nimeona niwachangie ili kuwarahisishia na kuwapunguzia makali kwenye usajili wao kwa kuwa hawana uongozi nimeona nichangie kupitia kwa mkuu wa mkoa kwa kuwa ni mdau wetu mkubwa wa soka nimetoa mchango shilingi milioni 10 ambazo nimeshazikabidhi tayari’’alisema Lingalangala.
Pia aliwaomba wadau wa michezo mkoani humo kujitokeza kwa wingi kuchangia timu hiyo’’Njombe mji na timu nyingine ambazo zipo mkoani kwetu ni timu zetu na hakuna mtu mwengine ambaye atatusaidia zaidi ya sisi wenyewe kupambana ili zifike mbali’’alisema Lingalangala.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya,alimpongeza mwenyekiti huyo kwa juhudi zake za kuhakikisha anahimarisha mchezo wa mpira wa miguu mkoani humo.
‘’Hamasa yake kubwa ni kuona mpira wa Njombe unakwenda kuongezeka ubora,mimi niseme kwa niaba ya uongozi na wanamichezo wote wa mkoa wa Njombe tunamshukuru sana dkt Lingalangala kwa mchango ambao ameutoa shilingi milioni 10 ambazo zinakwenda kusaidia katika usajili wa wachezaji’’alisema Rubirya.
Aidha alisema kuwa timu ya Njombe mji inakwenda kushiriki ligi daraja la pili na hivyo kuwataka wananchi wa Njombe kuona umuhimu wa kuunga mkono timu hiyo ili kuhakikisha inafika mbali.
‘’Tuchangie timu yetu ili kuhakikisha tunapata wachezaji wazuri kupitia mashindano mbalimbali ambayo yanaendelea na imani yangu kwamba tukitafuta vipaji kupitia mashindano hayo tutakuta na wachezaji wazuri ambao watakwenda kutengeneza timu imara ya Njombe mji’’alisema