Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe.Mustapher Siyani,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 24,2021 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Tume ya Utumishi wa Mahakama Bi.Enziel Mtei,akitoa maelezo mafupi kuhusu Mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 24,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akifatilia mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 24,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe.Mustapher Siyani,(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 24,2021 jijini Dodoma.
Katibu wa Kamati ya Maadili ya Mkoa wa Dodoma Bw.Vedastus Kilureti,akitoa taarifa ya jumla ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati,changamoto na mafanikio katika Mkoa wakati wa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 24,2021 jijini Dodoma.
Jaji wa Mahakam Kuu Kanda ya Temeke Mhe.Ilvin Mugeta,akitoa mada kuhusu muundo,majukumu na mamlaka ya tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Mikoa na Wilaya wakati wa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 24,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma,Mustapher Siyani amezitaka kamati za maadili za Mahakama za Mikoa na Wilaya kusimamia maadili ya mahakimu kwa kuhakikisha wanatenda haki katika utendaji kazi hususani mahakimu vijana.
Akizungumza leo Agosti 24,2021 Jijini Dodoma,Jaji Mfawidhi Siyani wakati akifungua semina kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maafisa wa kamati za Maadili Mikoa na Wilaya,amesema kamati hizo ni jicho la mahakama katika kusimamia maadili ya watumishi wa umma ili kuufanya mhimili huo uzidi kuheshimika.
“Ninafahamu umuhimu wa kamati hizi za maadili,kamati hizi ni jicho la mahakama katika kusimamia na kuendeleza maadili ya utumishi wa mahakama ili kuufanya mhimili huo uwe wenye kuvutia na kutukuka,”amesema Siyani
Vilevile, amesema kumekuwa na changamoto ya wananchi kuwa na uelewa mdogo kuhusiana na kazi na shughuli zinazofanya na kamati hizo,hivyo ametaka elimu itolewe ili jamii iweze kujua.
“Uzoefu tuliupata licha ya kamati kuwepo lakini malalamiko yamekuwa ni machache ila tumegundua ni uelewa mdogo katika kujua kama kuna Tume.Naiomba Tume iendelee kutoa elimu kwa njia mbalimbali ili kuwawezesha wananchi kufahamu uwepo wa kamati hizi
“Hali halisi inaonesha kwamba Mahakimu ni vijana jambo linalolazimika kujitafutia mali,naiomba Tume na Mahakama ziendelee kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama na kamati zitumie fursa chache ili kujiepusha na ukiukwaji huo na wawe watumishi waadilifu.
“Napenda ieleweke kusimamia uadilifu kwa afisa wa mahakama sio kuingilia uhuru wa mahakama binafsi nimefarijika kusikia suala hili lipo katika mada nini hasa umuhimu wa uhuru wa mahakama.Tumeamua kwa dhati kuhubiri uadilifu naombeni mtusaidie bila kumuoena wala kumuogopa mtu
Jaji Mfawidhi Siyani amesema kwa misingi hiyo kamati zinazowajibu wa kuzishauri Tume ya utumishi wa Mahakama kuhusu uzingatiaji wa maadili kwa maafisa wa Mahakama pamoja na uzingatiaji wa utoaji wa huduma bora na nafuu.
“Mada zitakazotolewa ni Muundo wa Tume ya Mahakama ni matumaini yangu mtajadili suala la utawala bora na mtapokea mafunzo hayo kwa umakini mkubwa lengo muwe na ufahamu mkubwa,”amesema
Jaji Mfawidhi Siyani amesema Kamati zinamsaada katika kusimamia maadili ya mahakimu hivyo anaipongeza Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kuweza kuwajengea uwezo kwani itawawezesha kutekeleza majukumu yao.
Amesema endapo kamati za Maadili zitafanya kazi vizuri maadili ya Mahakimu itaboreka na kuwawezesha wananchi kupata haki
Kwa upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gifti Msuya,amesema walipokea waraka kutoka Ofisi ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) nay a Wakuu wa Mikoa kwamba wanapaswa kuweka bajeti ya vikao hivi katika bajeti ya mwakaa ambapo amedai fedha hizo zimetengwa tangu mwaka jana.
Ameseme wataendelea kutekeleza na kusimamia kuhakikisha wale wanaoitwa katika kamati hizo wanatendewa haki na tuhuma zinakuwa za msingi
“Changamoto wananchi kuwa na uelewa mdogo juu ya kamati hizo jinsi zinavyofanya kazi hivyo mimi kama mwenyekiti nimejiwekea utaratibu wa kukutana na wananchi na kuwaelimisha juu ya hizi kama na jinsi gani wanaweza kuwasilisha malalamiko,”amesema Msuya
Naye Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Mahakimu Mkoa wa Dodoma Askofu Dickson Chilongani amesema amefurahi kupata mafunzo hayo kwani yamemsaidia kuweza kujua majukumu yake.
“Kwanza kabisa nimefurahi kuona Mahakimu ni sawa na sisi Maaskofu na wachungaji wana miiko yao na wana maadili ambayo wanatakiwa wazingatie na nimefurahi kuelezewa kazi zangu jinsi zilivyo,ikiwa ni pamoja na kusaidia mahakimu waweze kufanya kazi vizuri pamoja na kuwasaidia wananchi kama kuna shida waweze kuitumia kamati,”amesema.