Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Stephen Zelothe Stephen Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela na wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wakikagua barabara ya kiwango cha lami kipande cha Wasso Sale cha Kilomita 40.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Arusha Yasmin Bachu akishiriki shughuli za Kimaendeleo Katika Hospital ya Wilaya ya Ngorongoro.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa Neema Mollel sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro wakishiriki kazi za mikono katika Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro.
Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha Stephen Zelothe Stephen sambamba na Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Mkoa Gerald Munisi pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana Mkoa wa Arusha Ibrahimu Kijanga wakisaidia ujenzi hospital ya wilaya.
Wajumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha walipotembelea Gereza la Wilaya ya Loliondo kukagua mradi wa ukumbi wa Gereza hilo .
Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha Stephen Zelothe Stephen akishiriki ujenzi katika Chuo cha Ualimu Ngorongoro.
Wajumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Mkuu wa wilaya ya longido wakikagua ujenzi wa Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Longido.
Katibu wa Ccm Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka Sambamba na Mwenyekiti Zelothe Stephen wakishiriki ujenzi katika Hospital ya Wilaya.
Mwenyekiti Zelothe ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Mkoa ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi Wilayani Ngorongoro, ambapo amesema mradi wa barabara utakapo kamilika utaleta tija kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo kutokana na kufanya shughuli za usafiri kuwa rahisi pamoja na kufungua utalii zaidi.
Ujenzi wa mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami awamu ya kwanza wilayani Ngorongoro yenye kilomita 49 unatazamiwa kufungua fursa kwa wakazi wa wilaya hiyo na Mikoa ya jirani kutokana umuhimu wa barabara hiyo.
Katika hatua nyingine Serikali ya Chama cha Mapinduzi mkoani Arusha inatoa msimamo katika kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Tanroads Mkoa Masawe amesema Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 49 kutoka Wasso mpaka Sale kwa kiwango cha lami unatazamiwa kuifungua wilaya ya Ngorongoro na Mikoa ya Jirani katika sekta ya kiuchumi kutokana na urahisi wa usafirishaji pamoja na kuongeza fursa kwa watalii wanao fika katika eneo la ziwa Natron na Ngorongoro kwa lengo la kutalii.