Mgeni rasmi kwenye mahafali ya shule ya awali, msingi na sekondari Joyland Kigamboni Toangoma jijini Dar es Salaam, Bonaventure Mwambaja ambaye ni Mwanasheria wa TARURA Dar es Salaam akimsikiliza mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule hiyo, Rahim Hussein akielezea kuhusu fuvu la binadamu. Anayefuata ni Mkurugenzi wa shule hiyo, Fredrick Otieno.
Wahitimu wa darasa la saba wa shule ya Joyland ya Kigamboni Dar es Salaam wakiingia kwa mbwembwe kwenye mahafali ya shule hiyo ambayo yamefanyika leo Jumamosi kwenye viwnaja vya shule hiyo Toangoma Kigamboni
Wahitimu wanafunzi wa shule ya sekondari Joylanda iliyoko Toangoma Kigamboni Dar es Salaam wakiingia kwenye mahafalali shuleni hapo kwa mbwembwe
Wanafunzi wa shule ya awali Joylanda ya Toangoma Kigamboni Dar es Salaam wakionyesha umahiri wa kucheza nyimbo mbalimbali kwenye mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika siku ya Jumamosi kwenye viwanja vya shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya awali Joyland Toangoma Kigamboni Dar es Salaam wakionyesha umahiri wao wa mitindo ya mavazi kwenye mahafali ya shule hiyo siku ya Jumamosi shuleni hapo.
· Yawapeleka wanafunzi Mikumi, Kihansi na Udzungwa kujifunza kwa vitendo
Na Mwandishi Wetu
SHULE ya Joyland ya Toangoma jijini Dar es Salaam imeanzisha vilabu mbalimbali kwaajili ya kuvumbua vipaji vya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Hayo yalisemwa shuleni hapo siku ya Jumamosi na Mkuu wa Shule ya Msingi Joyland, Cyprian Maganga wakati wa mahafali ya shule ya awali, msingi na sekondari shuleni hapo.
Alisema wameanzisha klabu ya lugha, hesabu, sayansi, klabu ya uogeleaji, ya mapishi nay a muziki ambapo wanafunzi wenye vipaji wamekuwa wakipata nafasi ya kuonyesha umahiri wao kwenye maeneo hayo.
Alisema mbali na kuwakazania kitaaluma wanafunzi ni vyema shule kuwa na utaratibu wa kuvumbua vipaji vya wanafunzi kama Joylanda inavyofanya ili waweze kuvitumia kwa manufaa yao ya baadaye.
Alisema kwa sasa wanatafuta uwezekano wa kupata chumba cha kufundishia muziki ambacho gharama yake itafikia sh 15,000,000 hivyo aliwaomba wazazi wachangie upatikanaji wa chumba hicho kwa manufaa ya wanafunzi hao.
Alisema katika kuhakikisha Joyland itatoa mchango kwa jamii inasomesha watoto yatima 15 kwenye shule hiyo ambao walikuwa wanalelewa kwenye vituo vya yatima.
Alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakijiunza kwa nadharia na vitendo na shule zina kompyuta zisizopungua 60 na kwamba somo la haiba na muziki hufundishwa kwa vitendo na walimu waliobobea kwenye eneo hilo.
Alisema mbali na nadharia wamekuwa wakiwapeleka kusoma kwa vitendo na kwamba hivi karibuni wanatarajia kutembelea mbuga za Mikumi, kidatu, Kihansi, Kilombero Sukari na kwenye milima ya Udzungwa.
“Tunawaomba wazazi wote kuunga mkono ziara hizi za kimasomo ili watoto wenu wapate nafasi ya kujifunza kwa vitendo lakini pia kufanya utalii wa ndani,” alisema Maganga.