*********************************
Na Silvia Mchuruza,
Kagera.
Mamlaka ya Mapato Tanzania,mkoa wa Kagera ufafanuzi juu ya mabadiliko ya kodi kwa wafanyabiashara ambapo inategemea kukusanya shilingi bilioni 83 kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Akizungumza na wafanyabiashara hao wa manispaa ya bukoba afisa msaidizi ambayeanasimamia utoaji wa elimu na huduma kwa mlipa kodi mkoani kagera Alex Mwambenja kamesema kkuwa lengo la kutoa semina hiyo ni katika hali ya kukuza uchumi wa nchi
Bwana Mwampenja amesema kuwa kiwango hicho wanategemea kukipata kutoka kwa wafanyabiashara na walipa kodi wengine hivyo wanapaswa kuwa tayari kulipa kodi kwa hiari ili kujenga uchumi wa nchi.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha TRA inapanua wigo wa kukusanya kodi, katika mwaka wa fedha 2020/21 wamesajiliwa walipa kodi wapya elfu tatu na mpaka sasa zoezi hilo linaendelea .
Nao baadhi ya wafanyabiashara waliopata semina Alice Katabarwa na Justuce Kandokola wameshauri mamlaka hiyo kufanya marekebisho katika mfumo wao wa kukusanya kodi kwa njia ya mtandao na kuhakikisha maafisa wa kodi wanafika katika eneo husika na kujiridhisha kabla ya kumkadiria mtu kiwango cha kodi ya mapato.