Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge wa katikati akizungumza Jambo wakati alipofanya ziara yake Wilayani mkuranga kwa ajili ya kuzungumza na wakulima wa zao hilo.
*****************************
NA VICTOR MASANGU,PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge katika kukuza sekta ya kilimo ameamua kufanya ziara ya kuwatembelea baadhi ya wakulima wa zao la korosho Wilayani mkuranga kwa lengo la kuweza kusikiliza changamoto zao na kuweka mikakati ya kukuza zao hilo.
Kunenge katika ziara yake pia ametembelea shamba la Korosho la Mkulima Said Mbangwi lililopo katika eneo la Mkaliakitumbo kunionea mwenendo mzima wa maendeleo ya mkulima huyo.
Pia mkuu huyo wa Mkoa ameweza kufungua vikao vya wadau wa Tasnia ya Korosho Mkoani Pwani ambapo vitafanyika katika Wilaya tatu za Mkuranga, Rufiji na Kibiti.
Katika vikao hivyo vitalenga kuweka Mikakati kabambe ambayo itasaidia katika kuinua zao la Korosho na kuondoa Changamoto zinazolikabili zao hilo.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Flex Garden Mkuranga Kunenge alimshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa maelekezo yake ya kuhakisha Wakulima na mazao haya ya biashara yanatuletea tija
Kunenge alisema kuwa wamekutana kuzungumzia namna kuboresha uzalishaji na ubora wa Korosho za Pwani. Ameeleza kuwa Mkoa huo mwaka 2018/2019 ulizalisha Tani 23, 266.7 za korosho Mwaka 2020/2021 uzalishaji ulishuka hadi Tani 7, 0523 na ubora wake ulikuwa wa chini.
Ameeleza kuwa kushuka uzalishaji kumepekelea Kipato kinachotokana na Korosha kushuka kutoka Bilioni 31 hadi bilioni 7, “hii haikubaliki, Sisi Viongozi kama hatuwezi kusimamia zao la Korosho hatuna uhalali wa kuendelea kuwa kwenye majukumu haya” amesema Kunenge.
“Viongozi wetu Wakuu wamekwisha sema nini kifanyike, wanataka tuzalishe kwa wingi, Korosho yetu iwe Bora na impebbei nzuri Mkulima”.
Sisi wasaidizi wao tupo kuhakisha uzalishaji na ubora huo unafikiwa” alisema Kunenge.
Aidha aliongeza kuwa mkulima ambaye amepata fursa ya kunitembelea shambani kwake amemkuta anakabiliwa na changamoto ya kukosa wataalamu wa zao hilo.
”Wataalamu wetu wanatakiwa kuto Elimu ya kilimo cha Korosho na kwamba wanatakiwa wawe wanawatembelea kwa ajili ya kubaini changamoto zao,”alisema Kunenge.
Pia amewataka Wataalamu wa kilimo na Viongozi Mkoani hapo kubadilika. amewataka kumsaidia mkulima ili kuinua zao hilo.
Kunenge Amewataka wakulima kupalilia mashamba yao na kuachana na tabia ya kupeleka Korosho zenye ubora hafifu kwenye maghala.