Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira limetoa Mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 184 katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yenye lengo la kuwajengea uwezo juu ya mbinu za kubadilisha watu wenye mtazamo hasi juu ya maji, choo na usafi wa mazingira.
Mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 16,2021 yamefungwa Agosti 19,2021 katika kijiji cha Mwamala B kata ya Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga kwa kuwapa mafunzo hayo Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 wa kata hiyo,ikiwa tayari wahudumu 57 wa kata ya Mwantini na 53 kata ya Mwalukwa wamekwishapatiwa mafunzo hayo.
Afisa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika la LifeWater International, Bi. Truphina Ndungile amesema mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii ili kupata jamii yenye vijiji vyenye afya sambamba na kujikinga na magonjwa ya milipuko yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama, usafi wa mazingira pamoja na usafi binafsi.
Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa kwanza wa Shirika la LifeWater International unaojihusisha na maji safi na salama na usafi wa mazingira unaotekelezwa katika kata tatu ambazo ni Mwamala, Mwalukwa na Mwantini za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wenye lengo la kuwajengea uwezo wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii kwenda kubadili kaya zao ziwe na afya na jamii inayowazunguka ili kupata vijiji vyenye afya.
“Katika kipindi cha siku 4 tumetoa mafunzo kuhusu masuala ya maji safi na salama na usafi wa mazingira kwani tunataka wahudumu hawa wakatumie mbinu tulizowapa kutengeneza kaya zao ziwe kaya zenye afya na baada ya hapo wakatumie mbinu hizo hizo kwenda kutoa elimu kwa jamii. Tunapenda kuona kaya zina vyoo bora vinayozingatia viwango, kaya zimiliki na kutumia vyoo na kuacha kujisaidia kwenye maeneo ya wazi na maeneo yenye vyanzo vya maji”,amesema Truphina.
“Tunaamini kabisa kuwa wahudumu hawa wa kujitolea kwa kushirikiana nasi LifeWater International pamoja na Serikali ambayo tunashirikiana nayo watahamasisha jamii kupitia Programu ya Maono ya kijiji chenye afya ambayo inalenga kuvifanya vijiji vyote vilivyo ndani ya mradi kuwa na kaya zote zenye afya, zahanati na vituo vyote vyenye afya, shule zote zenye afya na taasisi zote za dini zenye afya”,ameeleza Truphina.
Pia amesema LifeWater International imetumia mafunzo hayo kugawa vitendea kazi yakiwemo mabegi, vitabu vya kufundishia na Tshirt zenye ujumbe wa “Mimi nina choo bora wewe je?” ili kuwarahisishia wahudumu hao wa kujitolea ngazi ya jamii kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuifikia jamii iliyokusudiwa kwa wakati ili kuleta mabadiliko chanya.
Nao Washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Raphael Jonas wamelishukuru shirika la LifeWater International kwa kuwapatia mafunzo hayo akisema wamefundishwa njia za kufanya jamii kuwa na kaya zenye afya, majukumu ya wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii, ufuatiliaji kaya zenye afya na umuhimu wa kutunza takwimu za kaya.
Amesema wamefundishwa kuhusu mbinu za kubadilisha watu wenye mtazamo hasi juu ya maji,choo na usafi wa mazingira, sifa za choo bora, umuhimu wa choo bora na kuzingatia usafi, umuhimu wa kunawa mikono, utunzaji wa maji na vyanzo vya pamoja na vyombo vya kutunzia maji.
Amesema pia wamefundishwa kuhusu Mwongozo na vigezo vya kaya yenye afya ikiwa ni pamoja na kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo, shimo la kutupia takataka, mazingira safi, afya ya mazingira na wanyama,karo la maji machafu na usafi binafsi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamala B, Hamis Philipo Izengo amesema mafunzo hayo yasaidia katika kuhakikisha vijiji vinakuwa na kaya zenye afya na kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kutumia ujuzi waliopata kusaidia jamii.
Naye Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Tom Mtitu amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO – 19 na kuwasihi kupata kwa hiari chanjo ya ugonjwa wa Corona ambayo inaendelea kutolewa nchini.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akizungumza wakati wa mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika kijiji cha Mwamala B, kata ya Mwamala.
Afisa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika la LifeWater International, Bi. Truphina Ndungile akizungumza wakati wa mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika kijiji cha Mwamala B, kata ya Mwamala. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Afisa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika la LifeWater International, Bi. Truphina Ndungile akizungumza wakati wa mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika kijiji cha Mwamala B, kata ya Mwamala
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Tom Mtitu akizungumza wakati wa mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo katika kijiji cha Mwamala B, kata ya Mwamala
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mwamala B, Kadashi Kadashi akizungumza wakati wa mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo katika kijiji cha Mwamala B, kata ya Mwamala
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamala B, Hamis Philipo Izengo akizungumza wakati wa mafunzo ya Pili kwa Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo katika kijiji cha Mwamala B, kata ya Mwamala
Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wahudumu wa Kujitolea ngazi ya jamii 74 kutoka kata ya Mwamala katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamala B, Hamis Philipo Izengo akimkabidhi mshiriki cheti cha kuhudhuria mafunzo ya wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii yaliyotolewa na Shirika la Life International
Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamala B, Hamis Philipo Izengo akimkabidhi mshiriki cheti cha kuhudhuria mafunzo ya wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii yaliyotolewa na Shirika la Life International
Sehemu ya wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii kata ya Mwamala wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kupokea vyeti vya kuhudhuria mafunzo ya wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii yaliyotolewa na Shirika la Life International
Wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii kata ya Mwamala wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kufungwa kwa mafunzo ya wahudumu wa kujitolea ngazi ya jamii yaliyotolewa na Shirika la Life International
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog