Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza leo Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu Mkoani Kigoma yenye urefu wa Kilometa 36 ambayo itagharimu bilioni 32.4
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa Wakandarasi wanaojenga mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu Mkoani Kigoma yenye urefu wa Kilometa 36 ambayo itagharimu bilioni 32.4
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze(kushoto) akitao maelezo leo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Tabora kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu Mkoani Kigoma yenye urefu wa Kilometa 36 ambayo itagharimu bilioni 32.4
Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Balozi Balozi Dkt. Batilda Buriani(katikati) akitoa ufafanuzi leo baada ya kuongozana na wajumbe wenzake kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu Mkoani Kigoma yenye urefu wa Kilometa 36 ambayo itagharimu bilioni 32.4
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Lucas Seleli(wa tatu kutoka kulia) akitoa ufafanuzi leo baada ya kuongozana na wajumbe wenzake kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu Mkoani Kigoma yenye urefu wa Kilometa 36 ambayo itagharimu bilioni 32.4
Picha na Tiganya Vincent
***************************
NA TIGANYA VINCENT
KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora imeomba kumlipa kiasi bilioni 2 Mkandarasi STECOL Corporation ambazo anadai kufuatia kazi alizokwishafanya katika mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu mkoani Kigoma.
Kauli hiyo imetolewa leo Wilayani Kaliua na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi wakati wa ziara ya Kamati kukagua miradi ya maendeleo,
Alisema Serikali inapaswa kumlipa kutokana na hati tatu ambazo ameshawasilisha ili kumwezesha kuendelea kwa kasi kwa kazi zilizobaki.
Aidha Mwenyekiti huyo alimtaka Mkandarasi kuhakikisha anajenga mapema na kiwango cha juu eneo korofi la Kazilambwa ambalo wakati wa masika linakuwa na maji mengi na wakati mwingine kusababisha kutopitika.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze(kushoto) alisema kuwa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 15 na unaurefu kilometa 36 na utagharimu bilioni 32,4 hadi kukamilika.
Alisema mradi huo umekuwa ukipenda polepole kutokana na uchelewashaji wa malipo kwa Mkandarasi hata baada ya kuwasilisha hati tatu(certificates)
Ndabalinze aliongeza kuwa mradi huo ulikuwa ukamilike Mwezi Novemba mwaka huu lakini hautakamika na hivyo wameomba Mkandarasi kuongezewa Miezi mitano.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema atawasiliana na Wizara ya ujenzi kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi ili kazi iendelee kwa kasi.