Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na muuzaji wa Gesi za Majumbani, Yona Kesi (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye maduka mbalimbali kwa wauzaji wa Gesi za Majumbani, kulia Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuber,ziara hiyo ilifanyika Agosti 18, 2021, jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani amepiga marufu tabia ya wafanyakazi wa shirika la umeme nchini (Tanesco) kukata hovyo umeme kwa madai kuwa gridi imetoka.
Dk. Kalemani ametoa onyo hilo jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua kituo cha kufua na kupoza umeme cha Zuzu.
Amesema, hivi sasa kumekuwa na tabia inayokera kwa watendaji wa shirika hilo kukata umeme hovyo bila kutoa taarifa kwa wateja kwa kisingizio cha gridi kutoka.
“Hapa Dodoma umeme kukatia ni marufuku lakini na shangaa juzi ulikatika ukiuliza unaambiwa eti gridi imetoka kwanini itoke na wewe upo hapo basi kuanzia leo tabia hii ikome kabisa kabla haijaondoka na mtu”amesema Dk. Kalemani
Amesema, hivi sasa mkoa wa Dodoma upo umeme wa kutosha kutokana na kuwepo kwa kituo cha kuafua umeme cha Zuzu ambacho kikikamilika kitakuwa na uwezo kuzalisha Megawati za umeme zaidi ya 600.
Amesema, mahitaji ya umeme kwa mkoa wa Dodoma hivi sasa ni Megawati 48, na yamekuwa yakipanda kila siku hivyo kituo hicho kitakua mkombozi kwa kuwa na umeme wa uhakika.
“Kituo hicho kinafua na kupoza umeme na kusambaza katika mikoa ya Singida lakini baadaye kitatumia pia kupeleka nchini Zambaia na Kenya”amesema Dk. Kalemani
Akizungumzia matukio ya kuungua kwa vituo vya kufua na kupozea umeme nchini amesema ipo haja ya kuwekwa kawa mifumo ya kubaini tatizo linaweza kujitokeza ili hatua zichukuliwe kabala ya kutokea.
“Lile tatizo la kituo cha kupoza umeme lililotokea hivi karibuni mkoani Morogoro tayari nimeshaunda tume ili kubaini kama ilikuwa bahati mbaya au makusudi”amesema
Aidha, amesema ili kukomesha hali ya kuungua kwa vituo hivyo Tanesco inatakiwa kuajili watumishi wenye uzalendo na wenye weledi katika nafasi hiyo.
“Hivi vituo ndipo umeme wote unatoka hapa tuweke watu wazalendo, wenye weledi na asiwe mlevi na nikikuta mtu mlevi yeye na aliye mwajili wote wataondoka na pia tusitumie raia wa kigeni hwa wanaweza kutunigiza chaka”alisema Dk. Kalemani
Meneja wa Mradi wa kituo hicho cha kufua umeme cha Zuzu Newton Mwakifwamba, amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika Septemba 27, mwaka huu.
“Mradi upo asilimi 98, za kukamilika na tunatarajia hadai kufikia Septemba 27, mwaka huu kuwa umekamilika na unaghalimu Dola za kimarekani milioni 53”amesema Mwakifwamba