Katibu Mkuu wa Chama Cha DP, Bw.Abdul Mluya akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa korona.
Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Bw.Doyo Hassan akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa korona.
Viongozi wa Vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi Bungeni wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mchakato wa katiba mpya na mwenendo wa utoaji chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa korona.
****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Umoja wa vyama vya siasa wasio na wawakilishi Bungeni wamesema wataendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu hasa kwa kauli yake ya kuwataka watanzania kuwa na subira kuhusu suala la mchakato wa katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Chama Cha DP, Bw.Abdul Mluya amesema kuna uwezekano wa kuendeleza pale walipoishia katika mchakato wa katiba mpya kuliko kuanza upya uandishi wa katiba kwa maana utaweza kupoteza gharama kubwa fedha ambazo zingeweza kuendeleza miradi mingine nchini.
“kwenye mchakato wa katiba tuliishia kwenye kura ya maoni (katiba pendekezwa) kwahiyo msimamo wetu tunasema kwamba kutokana na Dunia kuingia kwenye wimbi la ugonjwa wa korona uliopelekea kuyumba kwa uchumi hatuoni tija na afya kwa watanzania kama tutakwenda kuwaingiza kwenye suala uandishi wa katiba mpya kama ile iliyotumia zaidi ya bilioni 200”. Amesema Bw.Mluya.
Amesema kuna haja ya msingi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutuleta kura ya maoni tupige kura mwisho tuweze kupata katiba ambayo imeshatumia fedha za wananchi kuliko kuanza uppya mchakato wa kuandika katiba mpya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Bw.Doyo Hassan amewataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuikosoa chanjo ya kujikinga na Uviko -19 kwani chanjo hiyo inatolewa kwa hiari na haina madhara yoyote.
“Mheshimiwa Rais kwa busara zake ameruhusu kutoa mwanya kwa Watanzania wanaotaka na wasiotaka lakini yeye alikuwa ni miongoni mwa waliotaka na wakachanja na sisi viongozi tumemuunga mkono Rais katika chanjo ya Uviko kwasababu suala la afya linamuhusu mtu mmoja mmoja lakini kama taifa ukipoteza nguvu kazi ya taifa lazima upoteze harakati za kukuza uchumi wa taifa lako”. Amesema
Aidha amesema kuna haja ya kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuruhu msaada utufikie wa kupata chanjo hapa nchini ambapo msaada wa chanjo takribani milioni moja umeweza kufika nchini.