Vijana wa jeshi la akiba wilaya ya Ilemela wakiwa katika paredi ya kawaida kwaajili ya kumsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla akisaini kitabu cha wageni Cha kata ya Ilemela kabla ya kuanza kukagua gwaride la vijana wa jeshi la akiba na kuzungumza nao
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla wa pili kutoka kulia akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ilemela wakati wa kupokea taarifa fupi ya vijana wa jeshi la akiba wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla akizungumza na vijana wa jeshi la akiba wilaya ya Ilemela mwaka 2021
………………………………………………………………….
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla Leo Alhamisi ya Agosti 19, 2021 amefungua mafunzo ya jeshi la akiba wilayani humo yakihusisha vijana 77 wakiume 69 na wakike 8 kutoka kata mbalimbali zinazounda wilaya hiyo.
Akizungumza katika viwanja vya shule ya sekondari Lumala yanapofanyika mafunzo hayo, Mhe Masalla amesema kuwa anawapongeza vijana walioamua kujitoa na kujiunga na mafunzo ya jeshi la akiba kwani kitendo hicho ni cha kijasiri na kizalendo kitakachosaidia wilaya na nchi kwa ujumla kupata nguvu kazi na askari wa kulinda ulinzi na usalama wa nchi, raia na mali zao
‘.. Nawapongeza kwa mafunzo lakini utayari wenu wa kushiriki mafunzo haya kwa muda uliopangwa, Sisi tumekuja kwaajili ya kubariki Zoezi hili Kwa maana ya kufungua mafunzo, Ila kikubwa ni kusikiliza na kutii maelekezo yanayotolewa na viongozi wenu ..’ Alisema
Kwa upande wake mshauri wa mgambo wilaya ya Ilemela Afande … amesema kuwa mafunzo Kwa jeshi la akiba wilaya ya Ilemela yalianza mwezi Juni 14 mwaka huu ambapo vijana 88 walidahiriwa huku vijana 77 pekee wakisalia baada ya wengine kushindwa kuendelea na mafunzo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro na nidhamu
Aidha akaongeza kuwa vijana hao watapata mafunzo ya ukakamavu, mbinu za kivita pamoja na uraia mafunzo yatakayoendeshwa Kwa kushirikisha idara nyengine za ulinzi na usalama wakiwemo jeshi la polisi, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, jeshi la uhamiaji, jeshi la zimamoto na usalama wa taifa.