SPIKA wa Bunge Mhe.Job Ndugai,akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi mwakani kilichofanyika leo Agosti 18,2021 jijini Dodoma.
Spika wa bunge Mstaafu Anna Makinda, wakati wa kikao cha uhamasishaji wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi mwakani kilichofanyika leo Agosti 18,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi mwakani kilichofanyika leo Agosti 18,2021 jijini Dodoma.
Mtakwimu Mkuu wa serikali Dk. Albina Chuwa,akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi mwakani kilichofanyika leo Agosti 18,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai,akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi mwakani kilichofanyika leo Agosti 18,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameiagiza Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022.
Ndugai amesema hayo leo Agosti 18,2021 jijini Dodoma, wakati alipozungumza kwenye kikao cha uhamasishaji wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi mwakani.
Amesema elimu isipotolewa inaweza kusababisha kukwamisha zoezi hilo kwa sababu kuna baadhi ya makabila mila zake zinakataa kuhesabiwa watu wake ama mifugo yao.
“Jambo la Sensa ni muhimu sana watu kuhesabiwa lakini suala hili si jambo rahisi kwa sababu yapo baadhi ya makabila kama sisi wagogo kumuuliza mtu una wake wanagapi au mifugo mingapi ni ngumu sana hivyo elimu inahitajika sana ili kufanikisha zoezi hili” amesema
Pia, amesema elimu ikitolewa itaondoa mawazo na imani potofu iliyopo kwa baadhi ya makabila nchini kutokana na mapokeo ya kukataa kuhesabiwa kwa madai ya kuogopa kufa.
Kadhalika Ndugai amesema elimu inahitajika kwa makundi yote kabla ya kuingia kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema kikao hicho kimeshirikisha viongozi wa Dini, Siasa, Walemavu, wafanyabiashara, bodaboda.
Kundi lingine ni Wabunge,Wakuu wa wilaya ,Wenyeviti wa halmashauri,Wakurungenzi na maafisa mipango ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu hiyo na jumla ya washiriki nio watu zaidfi ya 500 waliohudhuria kikao hicho.
Mtakwimu Mkuu wa serikali Dk. Albina Chuwa amesema serikali inakusudia kufanya sensa yenye viwango vya juu tofauto na zilizopita.
Dk.Chuwa amesema katika zoezi la sensa ya watu na makazi ya sita itakusanya madodoso mengi na kuwashirikisha wananchi na makundi yote ili kupata takwimu sahihi kwa maendelkeo ya taifa.
Aidha, amebainisha kuwa zoezi hilo litatumia vishikwambi katika kukusanya taarifa mbalimbali kwa ajili kukukidhi mahitaji mengi ya serikali ili kuwahudumia wananchi.
Pia amesema sensa hiyo itakusanya taarifa za watu wenye ulemavu ili kujua idadi yao na serikali iweze kupanga bajeti kutokana ya kundi hilo.
Vilevile, alisema sensa ya watu na makazi mwakani itakuwa ya sita tangu nchi yetu imepata uhuru ambapo sensa ya kwanza ilikuwa mwaka 1967 na idadi ya watu ilikuwa milioni 12 na sensa ya pili ilikuwa mwaka 1978 idadi ya watu ilikuwa ni milioni 17.5.
Sensa ya tatu ilifanyika mwaka 1988 idadi ya watu ilikuwa ni 23.3 ,sensa ya nne ilikuwa mwaka 2002 idadi ya watu ilikuwa milioni 33.3 na sensa ya tano ilikuwa mwaka 2012 na idadi ya watu ilikuwa milioni 49.