Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mhandisi. Profesa. Sylvester Mpanduji akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya tatu ya wajasiriamali Kitaifa yanayotarajia kufanyika Septemba 21 hadi 30 mwaka huu katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
*****************************
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwa kushirikana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wameaandaa maonesho ya tatu ya wajasiriamali Kitaifa yanayotarajia kufanyika septemba 21 hadi 30 mwaka huu katika Wilaya ya Kasulu katika viwanja ya umoja Mkoani Kigoma.
Katika maoneshayo hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Dkt. Philip Mpango ambayo yamelanga kutoa fursa ya kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa na wanaviwanda, kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa wajasiriamali na wanaviwanda pamoja na kuonesha teknolojia mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mhandisi. Profesa. Sylvester Mpanduji, amesema kuwa maonesho ya mwaka huu wanatarajia kuwa na washiriki wajasirimali 500.
Profesa Mpanduji amesema kuwa hakuna kiingilio katika maonesho hayo, huku akieleza kuwa washiriki wataonesha teknolojia mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini pamoja na kuchochea katika kuanzishwa kwa viwanda vidogo na vya kati.
Amesema kuwa kunatakuwa na fursa za uwekezaji na kupata masoko na pamoja kukutana viongozi mbalimbali wa serikali, makampuni na wafanyabiashara wakubwa, wadau wa viwanda kama TMDA,TBS, BRELA, GS1, pamoja na taasisi za fedha.
“Wajasiriamali wote na wanaviwanda wanaalikuwa kushiriki maonesho haya kwa kuwa ndiyo fursa pekee ya kukuwezesha kutangaza bidhaa zako; kuuza; kukutana na wajasiriamali wengine kwenye fani yako na hivyo kujifunza zaidi; kukutana na wadau wa biashara; kupata oda; na kujionea teknolojia mbalimbali za usindikaji” amesema Profesa Mpanduji.
Amefafanua kuwa kauli mbiu ya mwaka huu katika maonesho hayo ni “PAMOJA TUJENGE VIWANDA KWA UCHUMI NA AJIRA ENDELEVU” ambayo yamelenga kumuinua mjasiriamali.
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) katika kutekeleza Sera ya Viwanda Vidogo (SME Policy) na Mpango Mkakati wa Shirika limekuwa likihamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa Viwanda Vidogo na vya Kati nchini.
Njia mojawapo ya kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda ni pamoja na kupitia maonesho yanayofanywa na SIDO Kitaifa na Kikanda, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini.
Katika kuhakikisha shughuli za shirika pamoja na bidhaa za wajasiriamali zinajulikana , njia mojawapo ni kupitia maonesho yanayofanywa na SIDO pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini.
Mwaka 2018, kwa mara ya kwanza SIDO kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, ilifanya maonesho ya kwanza kabisa ya SIDO Kitaifa ambapo zaidi ya wajasiriamali 600 na taasisi mbalimbali zilishiriki.
Kwa Mwaka 2019, SIDO ilifanya maonesho yake ya pili kwenye mkoa wa Singida kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Singida.
Takribani wajasiriamali 700 waliweza kushiriki maonesho hayo. Ushiriki wa wajasiriamali katika maonesho haya ulikuwa wa tija kwa kuwa bidhaa za wajasiriamali walio wengi waliweza kuuza, kupata masoko, kutengeneza mitandao, kupata huduma mbalimbali mubashara.
Kutokana na faida zilizoonekana kwenye maonesho ya Kitaifa yaliyopita na fursa mbalimbali zinavyoibuliwa, SIDO iliona ni vyema kukawepo na mwendelezo wa maonesho kwa mkoa utakaoomba.
Kwa mwaka huu 2021, SIDO kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma walituma maombi yao mapema baada ya maonesho ya SIDO Kitaifa Singida kumalizika na hivyo kupatiwa nafasi kwa mwaka huu.
Katika kuhakikisha maonesho hayo yanafanikiwa, mkoa umeandaa eneo la maonesho na kuhakikisha vitu kama umeme, maji, vyoo, mahema na vinapatikana. Pia mkoa unawahakikishia wajasiriamali wote watakaoshiriki usalama wa bidhaa zao katika kipindi chote cha maonesho.
Kamati ya maandalizi katika ngazi ya Mkoa itahusisha watendaji mbalimbali kutoka Ofisi ya RAS Kigoma, wakishirikiana na Mameneja wa SIDO kutoka kanda ya Kati (Singida, Katavi, Kigoma, Tabora, Dodoma).