MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza Halmashauri zote kuwa na Benki ya Tofali kwa kila Kijiji.
Alisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa pindi muda wa wanafunzi wanapotakiwa kijiunga na Darasa la Kwanza ama Kidato cha Kwanza.
Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Uyui.
Alisema kutokana na maoteo ya watoto wanatakiwa kiujiunga na Darasa la Kwanza kila Mwaka ni vema kuwepo na mipango endelevu la kukabiliana na ongezeko la watoto wanaingia Kidato cha kwanza kila Mwaka..
“Hatakiwa kuwa na mipango ya zima moto ya kusubiri watoto wachaguliwe ndio tuanze kufukuzana na ujenzi wa madarasa…tuweke mipango mizuri ya kutowafanya watoto wawe wanachelewa kujiunga na masomo eti kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarsa” alisisitiza