Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge wa kulia akikabidhi Mwenge maalumu wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla katika halfa iliyofanyika uwanja wa ndege terminal 1.
****************************
NA VICTOR MASANGU
Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo amekabidhi Mwenge maalumu wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Amos Makalla na kusema kwamba atahakikisha anaenzi kauli mbiu ya mwaka huu katika kupambana na madawa ya kulevya,afya na kutokomeza rushwa.
Kauli ya Kunenge ameitoa wakati wa tukio hilo la Makabidhiano lililofanyika katika Viwanja vya Ndege Dar es salaam Terminal I.
Awali Kunenge aliupokea Mwenge huo kutoka kwa Mhe. Mhandisi Martine Ntemo Mkuu wa Wilaya ya
Mafia.
Akitoa salaam fupi wakati wa Makabidhiano hayo Kunenge amesema, Mwenge huo umekimbizwa katika Wilaya zote saba na Kupitia Miradi 87, yenye thamani ya shilingi 57,314,068,446.
Ameeleza katika miradi yote iliyopitiwa ni mradi mmoja tu ulikataliwa kutokana na kukosekana kwa nyaraka, ameeleza kuwa wanafanyia kazi Maelekezo yote yaliyotolewa na Mkimbiza mwenge Kitaifa kwenye miradi hiyo.
Kunenge ameeleza pia katika mikesha ya Mwenge watu wengi walijitokeza na hivyo kutekeleza kauli mbiu zingine za kudumu za Mwenge ikiwepo kupambana na maambukizi ya VVU, kutokomeza Malaria, kupambana na Madawa ya kulevya na kupambana na Rushwa.
Mkuu huyo ameeleza Mkoa wake umetumia fursa ya mikesha ya Mwenge katika wilaya zote Saba ili kuwaelimisha wananchi pia kupima VVU
Kunenge alieleza kuwa watu 724 walipimwa na Kati yao watu 5 tu waligundulika kuwa na maambukizi ambayo ni sawa na asilimia 0.6.
Katika hatua nyingine aliongeza kwamba Watu WAPATAO 343 walipima malaria, na watu pia walipata fursa ya kuchangia damu kuchangia damu ambapo chupa 35 zilikusanywa.
Kadhalika hakusita kutoa elimu juu ya tahadhari ya UVIKO 19 na kuongezea kuwa hadi kufikia tarehe 16 Agosti 2021 jumla ya Watu 8328 walichanjwa.
Pia Kunenge amewapongeza wakimbiza Mwenge hao kitaifa kwa kuchapa kazi kwa weledi na kuweza kugagua miradi ya maendeleo katika ustadi wa hali juu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla amekiri kukupokea mwenge huo maalumu wa uhuru ukiwa salama pamoja na wakimbiza mwenge sita wa kitaifa.
Aidha aliongeza kuwa Katika mbio hizo Mwenge huo wa uhuru utaweza kutembelea katika jumla ya miradi mbali mbali ya .maendeleo ipatayo 46 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 100.