*****************************
18,agost
Na Mwamvua Mwinyi, Mafia
MWENGE maalum wa Uhuru ,umepitia miradi 12 yenye thamani ya milioni 95.885 ,wilayani Mafia, ambapo agost 18 mwaka huu, utakuwa umehitimisha Safari yake mkoa wa Pwani tayari kwa ajili ya makabidhiano Dar es salaam .
Akipokea mwenge huo kutokea Mkuranga ,mkuu wa wilaya ya Mafia ,Mhandisi Martin Ntemo alisema, kati ya miradi hiyo mmoja umezinduliwa ,kumi imetembelewa na mmoja kukaguliwa .
Akielezea mapambano dhidi ya rushwa ,-TAKUKURU wilaya ya Mafia kwa mwaka 2020/2021 imepokea taarifa 30 za vitendo vya rushwa,watu sita wamekamatwa kwa kuhusishwa na vitendo hivyo .
Ntemo alifafanua ,tuhuma 15 ziko katika hatua mbalimbali za uchaguzi na kuokoa milioni 25 .389.322 kutokana na chunguzi mbalimbali.
Pia alisema ,uongozi wa wilaya na Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau pamoja na wananchi wanaendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya ambapo hadi Juni 2021 jumla ya kesi 31 zimeripotiwa, huku 28 zikiwa zimefikishwa mahakamani na 3 bado ziko chini ya upelelezi .
Ntemo alifafanua kwamba, dawa za kulevya zilizokamatwa ni bangi kg.4.2, heroine gram 4.2 na wanaojihusisha na utumiaji ni 34.
Akitoa Ujumbe wa Mwenge , kiongozi wa mbio za mwenge maalum wa Uhuru ,LT.Josephine Mwambashi alikemea matumizi ya madawa ya kulevya na kutaka jamii kuwa washiriki wa kuwafichua wanaojihusisha na madawa ya kulevya na alikemea kupokea na kuomba rushwa.