KIUNGO mkabaji, Abdulsamad Kassim Ali amejiunga na mabingwa wa Tanzania, Simba SC kutoka Kagera Sugar ya Bukoba.
Mzanzibari huyo anayejulikana kwa jina la utani Guti akifananishwa na kiungo wa kimafaifa wa Hispania, José María Gutiérrez Hernández, ‘Guti’ anakuwa mchezaji mpya wa saba kutambulishwa kuelekea msimu ujao.
Wengine wapya ni beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda kutoka KMC ya Kinondoni, beki wa kati Mkongo Henoc Inonga Baka kutoka DC Motema Pembe ya kwao, Kinshasa, mawinga Msenegal, Msenegal Papa Ousmane Sakho kutoka Teungueth Rufisque ya kwao, Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba, Wamalawi, Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao, Blantyre na kiungo Duncan Nyoni kutoka Silver Strikers ya kwao, Lilongwe.

Kikosi cha Simba SC kipo kambini Jijini Rabat nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya.
Ikumbukee msimu ujao Simba itawakosa nyota wake wawili walioibeba timu kwa misimu miwili iliyopita, winga wa Msumbiji Luis Miquissone aliyeuzwa Al Ahly ya Misri na kiungo Mzambia, Clatous Chama aliyeuzwa RSB Berkane ya Morocco.