***********************************
Wakati tunaelekea kuuanza msimu wa 2021/2022, leo Agosti 15, 2021 Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na TFF zimefungua rasmi maombi ya vitambulisho maalum kwa ajili ya kuingia viwanjani (Accreditations). Zoezi hili litafungwa Septemba 5, 2021.
Tulikutana na changamoto kadhaa katika zoezi hili msimu uliopita, hivyo kwa pamoja tunapaswa kuhakikisha hazijitokezi tena msimu huu ili kupata ufanisi zaidi. Baadhi ya mambo ambayo yalikwamisha ama kuchelewesha zoezi msimu uliopita ni;
1. Baadhi ya Wanahabari ku’upload picha zisizofaa kwa ajili ya kitambulisho mfano selfie, picha zenye quality ya chini, picha zenye giza, picha zisizo na plain background na picha zisizokuwa katika mfumo wa passport size. Nawasihi kila mmoja wetu ahakikishe anaweka passport size inayofaa kwani maombi yatakayoambatanishwa na picha isiyofaa hayatashughulikiwa kabisa.
2. Picha ya kitambulisho cha kazi au Press Card ambazo hazionekani vema. Tuzingatie kuweka picha bora ambazo taarifa zilizomo zitasomeka vema ili watengenezaji wa vitambulisho wakamilishe kazi hiyo katika muda uliopangwa.
3. Wanahabari wengi walituma maombi zaidi ya mara moja. Ukisha’submit maombi yako, utapokea ujumbe usemao “Your application has been received, thank you.” Tafadhali usianze upya kujaza form au kupiga simu kuuliza kwani maombi yako yanakuwa yameshapokelewa. Kama kuna mahali unahisi umekosea, una nafasi ya kuhariri (edit) form yako kabla haijafanyiwa kazi.
Ni vema tukajaza form hii mapema bila kusubiri siku ya mwisho.
Mfumo hautapokea tena maombi baada ya Septemba 5, 2021.
Pia kwa upendo tuwatumie taarifa hii Wanahabari wenzetu wote popote walipo ili wasikose nafasi ya kuomba Accreditation.
Bonyeza link hii kujaza fomu;
https://forms.gle/8FmBt4PfvkFW32eYA