Mwenyekitiwa Jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Festo Kilipamwambu akiongea na wajumbe wa baraza la wazazi wa jumiya hiyo.Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi James Mgego akiongea na wajumbe wa baraza la wazazi la jumiya ya chama cha mapinduzi wilaya ya MufindiBaadhi Wajumbe wa baraza la wazazi wa jumuiya ya chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi
JUMUIYA ya wazazi ya
chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi imewataka wananchi na wanachama wa chama
hicho kuakikisha wanaenda kupata chanjo ya COVID 19 kwa lengo la kujikinga na
ugonjwa wa Corona.
Akizungumza kwenye baraza la jumuiya ya wazazi wa chama
hicho,mwenyekitiwa Jumuiya hiyo Festo Kilipamwambu alisema kunahaja ya wajumbe
wa jumuiya hiyo kwenda kupata chanjo hiyo kwa lengo la kujikinga kutoka na kuwa
na umri mkubwa.
Aliwataka wananchama wa
jumuiya hiyo kuzipuuza habari za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu juu
ya chanjo hiyo ambayo inasaidia kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Kilipamwambu alisema
kuwa ugonjwa wa Corona upon a unaua hivyo ni bora kuchukua tahadhari ya kupata
chanjo ambayo inasaidia kujikinga na ugonjwa huo ambao umekuwa janga kubwa la
dunia kwa ujumla.
“Naowaombeni sana
wajumbe wa jumuiya hii ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kuhakikisha
mnaenda kupata chanjo ya COVID 19 kwa lengo la kulinda afya zetu na kufikisha
ujumbe tuliwapa kwa wananchi wengine ambao hawaamini kuwa chanjo hiyo ni muhimu
kwao” alisema Kilipamwambu
kwa upande wake Katibu
wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi James Mgego aliwataka viongozi wa
jumuiya ya wazazi wa chama hicho kuhakikisha wanafika kwenye vikao husika kwa
lengo la kukijenga chama.
Alisema kuwa
walichaguliwa kwa lengo la kuhakikisha wanawawakilisha wanachama wengine kwenye
vikao kuanzia ngazi ya tawi hadi wilaya kwa lengo la kukijenga chama.
Mgego aliwataka wajumbe
wa jumuiya ya wazazi kuhakikisha wanahudhuria vikao vyote vya chama kwa
kufikisha maono ya wanachama wengi ambao hawawezi kuhudhuria vikao vya wilaya.
Alisema kuwa anaipongeza
jumuiya ya wazazi kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakiksha wanakijenga chama na
kufanikisha ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2020 kwa
kushinda nafasi zote.