Home Mchanganyiko CCM YASHIRIKI KUSAMBAZA TABASAM KWA WATOTO WENYE SARATANI NCHINI

CCM YASHIRIKI KUSAMBAZA TABASAM KWA WATOTO WENYE SARATANI NCHINI

0

*************************

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Godfrey Chongolo leo tarehe 15 Agosti, 2021 ameshiriki matembezi ya Km 5 yalioandaliwa na Benki ya CRDB yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kugharamia matibabu kwa watoto wenye Saratani na utunzaji wa mazingira nchini.

Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Green Park Osterbay ambapo Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

CCM imeshiriki kusambaza tabasam kwa watoto wenye Saratani, CCM imeshiriki utunzaji wa Mazingira

Imeandaliwa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI