Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkongo alipotembelea Kituo cha Afya katika Kata hiyo Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
*****************************
Na Mwandishi Wetu Namtumbo
Wananchi wa Kata ya Mkongo Kata ya Mkongo Wilayani Namtumbo wameiomba Wizara Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kukarabati na kuwapatia wahudumu katika kituo cha Afya Mkongo ambacho kinahudumia Kata Sita.
Hayo yamebainikia wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Akizungumza mara baada ya kusikiliza kero hiyo Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewaahidi wananchi hao kulitatua tatizo hilo la ukaratabi wa majengo na upungufu wa wahudumu wa Afya.
“Nimeona hali halisi katika kituo hiki cha afya umbali kufika hapa huduma hii ni muhimu sana hili tutalifanyia kazi “alisema Mhe. Mwanaidi
Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewahakikishia Wazee kupata huduma za Afya kwa kipaumbele katika vituo vya Afya kwani ni kundi maalum linaloaangaliwa na Serikali kwa ukaribu.
Kituo hicho cha Afya kina zaidi ya miaka thelathini hakijafanyiwa uakarabati mkubwa na kiahudumia wananchi wengi zaidi ya uwezo wake.