Waziri wa viwanda na biashara ,Profesa Kitila Mkumbo akiwa amefuatana na wabunge wa kamati ya bajeti walipotembelea kiwanda cha A to Z kilichopo Kisongo mjini hapa (Happy Lazaro)
Waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watendaji wa kiwanda cha A to Z kilichopo mjini hapa alipotembelea akiwa amefuata na kamati ya Bunge ya bajeti (Happy Lazaro)
Meneja masoko wa nchi za nje kutoka kampuni ya A to Z, Sylvester kazi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kutembelea kiwanda hicho .(Happy Lazaro)
***************************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Wizara ya viwanda na biashara kuiomba Bunge kuridhia nchi ya Tanzania kujiunga na mkataba wa biashara huru wa Afrika kutokana na ushindani mkubwa uliopo katika nchi za Afrika .
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa viwanda na biashara ,Profesa Kitila Mkumbo wakati alipofanya ziara katika kiwanda.cha A to Z akiwa ameongozana na kamati ya Bunge ya bajeti inayoendelea na ziara yake mkoani Arusha.
“wizara ina mpango wa kuomba Bunge liridhie Tanzania kujiunga na mkataba wa biashara huru wa Afrika kwani viwanda vinahitaji ushindani mkubwa ndani ya Afrika na Dunia kwa ujumla na kwa kufanya hiyo tutaweza kupanua wigo mkubwa katika kufanya biashara zetu na kwa viwango vikubwa zaidi.”amesema Profesa Mkumbo.
Profesa Mkumbo amesema kuwa, endapo Tanzania ikisaini mkataba huo itasaidia kufungua masoko katika nchi 54 za Afrika.
Ameongeza kuwa,kuhusiana na kamati ya Bunge ya bajeti mambo watakayosaidia ni kuhusu kodi katika kujenga hoja kuishauri wizara ya fedha kuona kwamba Kodi wanazoziweka ziwe ni kodi ambazo zinachochea uzalishaji katika viwanda pamoja na kuweza kushindana katika soko la ndani ya nchi na ukanda wa Afrika.
Kwa upande wake Meneja masoko wa nchi za nje kutoka kiwanda Cha A to Z Sylvester Kazi amesema kuwa, changamoto kubwa zaidi inawayokabili ni marejesho ya VAT ambayo yamechelewa sana ambapo wameiomba kamati iweze kusaidia fedha hizo ziweze kutoka kwa wakati ili waweze kuwekeza na kuongeza uzalishaji zaidi.
Ameswma kuwa, changamoto nyingine ni ongezeko la kodi kwenye nyuzi za pamba kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 25 ambapo ,wameiomba serikali kurudisha kwenye kiwango cha awali kwani kuna mikataba ya mauzo ambayo walishaingia na haiwezekani kuongeza Bei ya bidhaa hizo tena, hali inayohatarisha ustawi wa kiwanda kutokana na kutarajia kupata hasara.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti, Daniel Baran amesema kuwa ,wamesikia changamoto hizo na Kama kamati wamezichukua ili kwenda kushirikiana na serikali kuutafuta ufumbuzi kwani kiwanda hicho ni moja kati ya viwanda vinavyofanya vizuri katika ulipaji wa kodi ambapo kwa mwaka wanalipa zaidi ya bilioni 17.
Amesema pamoja na ulipaji wa kodi pia kiwanda kimeajiri zaidi ya watanzania 800 hivyo kamati imejionea uhalisia wa bidhaa wanazozizalisha ambapo wameelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuwaandikia changamoto hizo rasmi ili waweze kuzichambua na kuona katika bajeti ijayo ni namna gani serikali itaingilia kati na kubadilisha viwango hivyo vya kodi.