Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa mradi wa East Africa for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP).Dkt.Erick Mgaya akiwa na waandishi wa habari wakikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha kipekee cha umahiri cha kikanda katika nishati jadidifu (EASTRIP) kinachomilikiwa na Chuo Cha Ufundi Arusha eneo la Kikuletwa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa mradi wa East Africa for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP).Dkt.Erick Mgaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua na kujionea mradi wa ujenzi wa kituo cha kipekee cha umahiri cha kikanda katika nishati jadidifu (EASTRIP) kinachomilikiwa na Chuo Cha Ufundi Arusha eneo la Kikuletwa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Muonekano wa Bwawa lililokuwa mradi wa uzalishaji umeme ambap kwa sasa linakarabatiwa na kuwa kituo cha kipekee cha umahiri cha kikanda katika nishati jadidifu (EASTRIP) katika eneo la Kikuletwa kinachomilikiwa na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kilichopo Hai Mkoani Kilimanjaro.
Muonekano wa jengo la Utawala lililopo Kikuletwa wilayani Hai Mkoani Kilimanajaro.
…………………………………………….
Na.Alex Sonna,Hai
WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeendelea kuboresha miundombinu katika mradi wa kituo cha mafunzo ya kufua umeme kwa kutumia nguvu za maji cha Kikuletwa kinachomilikiwa na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kilichopo Hai Mkoani Kilimanjaro .
Kituo hicho kitasaidia katika mafunzo ya jinsi ya kuongeza uzalishaji wa umeme unaotokana na maji katika maeneo mbalimbali nchini ambapo pia kitaendelea kuzalisha wataalamu waliobobea katika fani ya kufua umeme.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa mradi wa East Africa for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP).Dkt.Erick Mgaya amesema gharama ya Project hiyo ni shilingi bilioni 37 ambapo kituo cha Kikuletwa kimechaguliwa katika umeme Jadidifu.
“Gharama ya Project ni shilingi bilioni 37 na kwenye Project ya World Bank ambako Serikali imechukua mkopo Wizara ya Elimu ina Centre nne Tanzania, sisi tumechaguliwa katika Renewable Energy,DIT Kwa kiwango hicho hicho cha fedha wamechaguliwa kwenye mambo ya TEHAMA
“ DIT Campus ya Mwanza kwa kiwango hicho hicho cha fedha kwenye wao wamechaguliwa katika Agroproduct hasa wao wapo kwenye masuala ya ngozi na NIT Transportation na Logistical wao wana kiwango kikubwa zaidi kwa sababu wameenda mpaka katika usafiri wa anga wana vifaa vingi vya kununua,”amesema.
Amesema kupitia mradi huo wanatarajia kujenga Hosteli mbili ya kuchukua wasichana 500 na wavulana 500 ambapo pia watajenga work shop sita,jengo la utawala,nyumba za watumishi,Dispensary na sehemu ya kulia chakula.
“Kwa sasa tuna kituo cha kutunza wanafunzi 64 lakini tumeongeza mabweni mengine mawili ambayo yanaweza kuchukua wanafunzi wengine 52 tutakuwa na wanafunzi 168 ambao wanaishi katika chuo,”amesema.
Akizungumzia malengo makuu ya mradi huo ni kuboresha utoaji wa elimu ya ufundi ili kuongeza idadi ya wahitimu wa elimu ya ufundi, kuboresha mbinu za ufundishaji na kuboresha mitaala na kuwezesha ulinganifu wa elimu ya Ufundi katika eneo la Afrika ya mashariki.
“Kinachofanyika huko ni kuboresha masuala ya utawala,kwa kuajiri baadhi ya wataalamu,tumeweza kuanzisha kamati za ushauri kutoka viwandani,Kuboresha mafunzo kwa kuanzisha mitaala mipya ya nishati Jadidifu,kila Programu ina malengo yake na hakuna chuo ambacho kinatoa mafunzo na sehemu ya kufanyia mafunzo
“Kwa kutumia hichi wengi wanajifunza tumeishaongea na Tanesco hata kuwapa mafunzo wafanyakazi wao Vilevile maeneo ya Makambako tumeanza kufanya upembezi yakinifu kuzalisha umeme kwa kupitia upepo hivyo ni lazima tuzalishe wataalamu wengi ,Wengi watanufaika viwanda na majirani nao watanufaika
“Mpaka sasa kituo tayari kinafanya kazi na baadhi ya Programu zinaendelea kufanya kazi kwani tuna Programu sita,Tutakuwa tumeongeza ubora wa bidhaa mbazo tunazalisha katika nishati Jadidifu tunaongeza uwezo wa watumishi na tunawapeleka kujifunza kwa vitendo na watajua mashine zinavyofanya kazi,”amesema.
Amesema Kituo cha Kikuletwa kimetengewa jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 16.25 (TShs. 37.4 Bilioni), kwa ma tumizi ya Kuboresha na kuimarisha uongozi na usimamizi wa shughuli za kituo (5.3%),Kurasimisha ushirikiano baina ya Chuo na waajiri/viwanda katika kutoa mafunzo ya ufundi, ikiwemo kutumia wakufunzi kutoka viwandani na mashine za viwandani kwa mafunzo (4.2%).
Pia,Kuandaa mitaala mipya inayoendana na mahitaji ya soko la ajira (2.1%),Kutoa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa wakufunzi katika kufundisha mitaala mipya na utoaji mafunzo kwa njia za kisasa. Mafunzo hayo yatatolewa kwa kozi za muda mrefu na muda mfupi (5.3%),Kuimarisha miundo mbinu iliyopo ya kufundishia na kujenga miundo mbinu mipya, ikiwemo ujenzi wa majengo na ununuzi wa vifaa vipya vya kufundishia (80.9%).