Home Mchanganyiko MMILIKI WA FULLSHANGWE MEDIA AJITOKEZA KUPATA CHANJO YA KUJIKINGA NA COVID-19

MMILIKI WA FULLSHANGWE MEDIA AJITOKEZA KUPATA CHANJO YA KUJIKINGA NA COVID-19

0

Mhariri Mkuu na Mmiliki wa Full Shangwe Media Bw. John Bukuku akipata chanjo ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo Agosti 12,2021.

***************************

Mmiliki wa Fullshangwe Media bw.John Bukuku amejitokeza kupata chanjo ya kujikinga na ugonjwa  wa Corona katika viwanja vya karimjee Jijini Dar es Salaam na kuwahimiza watu wengine kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata chanjo.

Amesema kuna uvumi katika maeneo mbalimbali hasa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vijiwe wakisema kuwa chanjo hiyo si sahihi na ina madhara kitu ambacho si kweli hivyo amewataka wananchi kupuuza uvumi huo.

Serikali kupitia Wizara yya Afya imeruhusu wanachi wote kupata chanjo kuanzi wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.