MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 akiwa na bango la kuhamasisha uvaaji wa barakoa na wananchi kuhakikisha wanachanja |
MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 wa kwanza kulia akiwa kwenye picha na Waziri wa Afya Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto
MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 akifuatiwa na
Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria.
Mbunge Neema Lugangira ameteuliwa kuwa Balozi wa harakati za kupambana na Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (Balozi wa UVIKO19 – COVID19).
Mbunge Neema Lugangira ameteuliwa Alhamisi ya Agosti 12 mwaka huu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Dk. Dorothy Gwajima Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Mbunge Neema Lugangirq, wengine walioteuliwa ni Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria.
Tangu janga la UVIKO 19 (COVID19) liingie nchini kwenye Wimbi la Kwanza hadi sasa Wimbi la Tatu, Mbunge Neema Lugangira ameonyesha kupambana na janga hilo huku akielimisha na kuhamasisha Watanzania kujikinga na kuchoma Chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari duniani wa COVID19.