Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla akihutubia wananchi wa kata ya Nyasaka mkutano uliofanyika katika viwanja vya Sokoni
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasana Elias Masalla akizungumza na walimu wa shule ya sekondari Nyasaka alipofika kusikiliza kero zao
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla akikagua ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Nyasaka
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasana Elias Masalla akisikiliza kero na changamoto za watumishi wa afya katika zahanati ya Kiloleli
******************************
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla amefurahishwa na jitihada za mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula katika kuunga mkono Serikali juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya hiyo
Mhe Masalla amezungumza hayo akiwa kata ya Nyasaka viwanja vya soko jipya ikiwa ni tamati ya ziara yake kwa awamu ya kwanza iliyohusisha kutembelea kata kumi kwaajili kusikiliza kero za wananchi, kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kukagua miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa, kuhamasisha wananchi juu ya kuchukua tahadhari za ugonjwa wa UVIKO-19 ambapo amesema kuwa anafurahishwa na juhudi za mbunge huyo katika kuiunga mkono Serikali katika kumaliza kero za wananchi kwa kutekeleza miradi yenye tija kwa watu wake, Ambapo wananchi hujenga misingi, Mbunge hutoa tofali za kukamilisha maboma ya miundombinu hiyo na Serikali kupitia manispaa kumalizia, Sera ambayo imepewa jina la “utatu”
‘.. Mfikishieni salamu zangu Mhe Mbunge, Na Mimi mwenyewe nitamtafuta najua ana majukumu ya Kiserikali, Serikali inafurahishwa kuona namna anvyounga mkono jitihada za maendeleo maana kila tulipopita tumeona mkono wake ..’ Alisema
Aidha mkuu wa wilaya huyo akawatoa hofu wananchi wa kata ya Nyasaka juu ya changamoto ya upatikanaji wa maji kwa uhakika ambapo amesema kuwa baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa tanki kubwa la maji la Buswelu lililogharimu zaidi ya bilioni tano adha hiyo itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa kama si kuisha kabisa huku akimshukuru Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo
Nae mwakilishi wa mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni afisa ardhi na mipango miji Shukran Kyando akawaasa wananchi hao kuendelea kuchukua tahadhari na ushauri unaotolewa na wataalam wa afya dhidi ya ugonjwa UVIKO-19 huku akisisitiza kufatwa kwa sheria na taratibu za mipango miji katika matumizi ya ardhi sanjari na kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na mkuu huyo wa wilaya
Kwa upande wake kamanda wa polisi wa wilaya ya Ilemela SSP Elisante Ulomi amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya uharifu na kuongeza umakini katika matumizi ya mitandao kwani kumekuwepo na ongezeko la wizi wa kimtandao
Beatrice Daudi ni moja ya wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao kwa mkuu huyo wa wilaya ambapo amelalamikia vitendo vya uharifu katika mtaa wa Nyamuge ndani ya kata ya Nyasaka wakati Joseph Peter akilalamikia kukosekana kwa huduma ya maji ya uhakika.