*******************************
Kiungo wa klabu ya Simba Sc na timu ya Taifa ya Zambia Clatous Chama akiwa pamoja na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga Mkongo Tuisila Kisinda wamejiunga na klabu ya RSB Berkane inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco.
Wachezaji hao ambao wamefanya vizuri kwenye klabu zao ndani yya ligi kuu Tanzania bara sasa watacheza timu moja na kuitumikia klabu hiyo ya nchini Morocco katika msimu ujao wa 2021/2022.
Simba Sc ipo kwenye hatua za mwisho pia za kumuuza nyota wake kutoka Msumbiji, Luis Miquissone kwenda Al Ahly ya Misri, wakati kiungo Mkongo wa Yanga, Tonombe Mukoko anaweza kuondoka pia.