**********************************
Na Farida Saidy Morogoro.
Wafugaji Wavamizi, Wakulima, pamoja na Wavuvi katika Kijiji cha Tulo Kilichopo Wilaya ya Morogoro wamesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira katika mto Mvuha kutokana na wafugaji kupitisha mifugo katikati ya mto kama njia, wakulima kuchepusha maji kwa ajili ya Kilimo na Uvuvi, huku mto huo ukiwa unategemewa kupeleka maji yake kwenye mto ruvu ambao unatumika kuzalisha maji yanayotumiwa na mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani.
Mamlaka ya bonde la Wami Ruvu imefika na kujionea uharibifu huo mkubwa wa mazingira kwenye mto huo ikiwemo uoto wa asili ukiwa umeondolewa kabisa kutokana na shughuli za ufugaji na kilimo, huku hali hiyo ikihatarisha maji kupungua kwa kiasi kikubwa katika mto huo hasa kipindi cha kiangazi.
Akizumza mara baada ya kujionea uharibufu uliofinyika katika mto huo Mhandisi wa Mazingira Bonde la Wami Ruvu. Mhandisi Abdalah Mshana amesema uharibifu ulifanyika katika mto huo umeathili upatikanaji wa maji katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kufanya shughuri za kibinaadamu kwenye vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha uharibifu wa mazingira na kupoteza uoto wa asili.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Tulo Bwana Mohamed Mkange amesema wanakumbana na changamoto nyingi katika kulinda mto huo ikiwemo kupigwa na wafugaji pamoja na ujeuri wa wananchi juu ya utunzaji wa eneo hili.
Nao wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na mto huo wameeleza namna wanavyokutana na changamoto za uhifadhi wa mto huo ikiwemo ufugaji na uvuvi ambao wamekuwa wakitumia nguvu nyingi katika kukabiliana nao kwenye utunzaji wa mto huo.