Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika leo Agosti 12,2021 Jijini Dodoma
Baadhi washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika leo Agosti 12,2021 Jijini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Patrobas Katambi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki katika maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika leo Agosti 12,2021 Jijini Dodoma
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana kujituma katika kufanyakazi na kuacha tabia ya kufikiria maisha mazuri
Katimbi ameyasema leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma wakati alipozungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya siku ya vija na Kimataifa .
Katambi amewataka vijana nchini kujituma kazini ili kufanikiwa kimaisha na kuacha tabi ya kulalamika vijiweni na kutafuta maisha bora bila kufanyakazi
“Tunajua ajira ni chache lakini kazi zipo nyingi unaweza kujiajiri mwenyewe kwa njia ya kilimo au kufanyabiashara hivyo tuondokane na malalamiko kuhusu ajira”alisema.
Kadhalika amesema kuwa kazi ya Serikali ni kumwekea mazingira mazuri watu wake ili waweze kuzalisha uchumi na haiwezi kuajiri kila raia wake .
Hata hivyo amewahakikisha vijana wanawezeshwa kiuchumi kupitia halmashauri kuna fungu limetengwa kwajili ya mikopo yao lakini wanatakiwa kuunda vikundi.
Amesema kuwa Serikali inaungana na Jumuiya ya kimataifa katika kuthamini mchango wa Vijana katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii kutokana na kushiriki kwao kikamilifu katika shughuli za Maendeleo ya Kiuchumi, kisiasa na kijamii.
“Dhumuni kuu la kuadhimisha siku hii ni kuiwezesha Jumuiya ya Kimataifa na jamii kwa ujumla kupata fursa ya pamoja ya kusherehekea na kutambua nafasi ya Vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Nchi zao”amesema Katambi
Aidha amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhesimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuwawezesha vijana kujiendeleza kupitia ubunifu ambapo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii lakini pia vijana wamekuwa wakihimizwa kutumia Ubunifu wao kujiajiri.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA, Dkt. Mariam Ngaeje amesema takwimu zinaonesha kwamba kuna vijana bilioni 1.2 duniani wenye umri kati ya miaka kuanzi 10 hadi 19 duniani kote kati ya hao milioni 207 sawa na asilimia 17.3 wanakabiliwa na tatizo la uzito uliokithiri.
Dkt. Ngaenje amesema kuwa zaidi ya vijana 1.8 bilioni wenye umri umri kati ya miaka 15 hadi 24 wanaishi katika nchi zinazoendelea na nusu yao wanafanya kazi katika sekta ya kilimo na chakula.
Pia amesema kuwa kwa mbali na hayo watoto wa kike wapo katika hatari zaidi ya kupata utapiamlo kutoakana na athari za mila na desturi ambazo usababisha ukosekanaji wa vyakula vyenye virutubisho,elimu bora na fursa za Kiuchumi.
“UNFPA pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ikiwemo UNICEF, UNESCO, UNAIDS, WHO na ILO tutaendeelea kushirikiana na serikali pamoja na vijana na wadau wengine katika kuleta maendeleo na kufanikisha malengo mbalimbali ya vijana Tanzania,” amesema Ngaeje
Dk.Ngaeje amesema kuwa UNFPA imedhamilia kusaidia vijana na taasisi zao kama ilivyobainishwa vizuri katika mkakati wa UNFPA wa vijana unaoitwa “My Body ,My life,My World”.
Aidha amesema kuwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Kimataifa uliofanyika mwaka 1999 ulipanga kuwa tarehe 12 ya Augosti kila mwaka itakuwa maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa na hadi leo maadhimisho hayo yamefikisha miaka 22.
Awali akiwasilisha maazimio kwa niaba ya vijana Bi. Rabia Mussa amesema vijana wanaiomba serikali kutoa miongozo kwa halmashauri na mashirika ya umma kutangaza fursa kama vile zabuni ikiwa ni pamoja na kuweka msisitizo katika maeneo ya mbalimbali ili wanufaike na fursa kupitia ujuzi na ubunifu walionao katika kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kama ilivyoainishwa kupitia mpango wa miaka mitano wa maendeleo wa taifa 2021/22 mpaka 2021/2025.
Maadhimisho ya Siku Kimataifa ya Vijana huadhimishwa kila Mwaka tarehe 12 Agosti na mwaka huu 2021 yamebeba kauli mbiu isemayo “Ubunifu na Ushiriki wa Vijana katika Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”.